Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil. 6 zatumika ujenzi chuo cha uhasibu Mtwara

Bil. 6 Zatumika Ujenzi Chuo Cha Uhasibu Mtwara Bil. 6 zatumika ujenzi chuo cha uhasibu Mtwara

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mtwara wameishukuru serikali kwa kukamilisha ujenzi wa chuo hicho kilichogharimu shs bilioni 6 hadi kukamilika wakisema wameondokana na changamoto iliyokuwa ikiwakabili kabla ya ujenzi huo.

Wakizungumza wakati wa kutolewa taarifa kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa chuo, baadhi ya wanafunzi wamesema kabla ya ujenzi walikuwa wanapata changamoto ya usomoji kutokana na miundombinu ya madarasa kutokuwa rafiki na ukosefu wa vitendea kazi kama vile kompyuta.

Wametoa raia kwa wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini kujiunga na chuo hicho kwani miundombinu ya kusomea ni mizuri na ya kisasa.

Mkurugenzi wa TIA Kampasi hiyo ya Mtwara Dk. Godwin Mollel amesema kukamalika kwa ujenzi huo kutaenda kuongeza idada ya uandikishaji kwa wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali nchini.

"Kukamilika kwa ujenzi huu kutawafanya wanafunzi kusoma kwenye mazingira mazuri ambayo yameboreshwa na kutasaidia wanafunzi kupata nafasi ya kujiunga na chuo hicho hususani kanda ya kusini Lindi, Mtwara na Ruvuma,"amesema Mollel.

Kabla ya kukamilika kwa ujenzi chou hicho kililikuwa kinatumia majengo ya kukodi na kusajili wanafunzi 1,000 lakini sasa chuo kina uwezo wa kusajili wanafunzi zaidi ya elfu 2,000 kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live