Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil 6/- zatengwa kurejesha uoto wa asili

0b82d25bf30bad14c0c2f34458df1b46 Bil 6/- zatengwa kurejesha uoto wa asili

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetenga Sh bilioni sita kwa ajili ya kurejesha uoto wa asili ambao utasaidia kuotesha miti ya matunda na ile ya asilia ambayo imeanza kutoweka.

Hayo yalisemwa na Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdullah wakati akifunga Maonesho ya Kilimo maarufu Nanenane huko Dole Kizimbani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Alisema serikali imejipanga kuweka miundombinu ya kisasa ya sekta ya kilimo na kurudisha hadhi ya Zanzibar katika uzalishaji na usafirishaji wa mazao ya kilimo kibiashara zaidi.

Aliitaja mikakati inayotarajiwa kuchukuliwa na serikali ni pamoja na kuwekeza katika umwagiliaji wa mpunga.

Aidha, Abdullah alisema serikali imeweka mikakati ya kuimarisha sekta ya mifugo na kuona wananchi wanafuga kwa kutumia mbinu za kisasa zitakazoingiza mapato na kujiajiri.

Aliitaja mikakati inayotarajiwa kuchukuliwa na serikali ni pamoja na ununuzi wa mtambo wa uzalishaji wa gesi ya Nitrogen kwa ajili ya kuhifadhi mbegu za kupandishia ng’ombe kwa njia ya sindano.

''Uzalishaji wa sekta ya mifugo umeshuka kwa kiwango kikubwa na kupoteza mwelekeo ambapo mikakati yetu tunataka kuona mifugo inatoa ajira kwa vijana na kuinua uchumi wao,'' alisema.

Mapema Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis alisema maonesho ya kilimo yameonesha mafanikio ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo za matunda.

Alisema Idara ya Kilimo kupitia Kituo cha Utafiti wanaendelea na utafiti wa mbegu za mazao kuona ubora wake na uzalishaji ikiwemo muhogo, magimbi pamoja na viazi vitamu.Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM), Azania Msingiri alisema wameitikia wito wa serikali wa uchumi wa buluu na kuvua katika maeneo ya bahari kuu na kuvuna rasilimali yaWahimizwa kujitokeza kwa sensa

Chanzo: www.habarileo.co.tz