Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil. 5.14/- ushuru forodha hazikuthibitishwa

KONTENA Bil. 5.14/- ushuru forodha hazikuthibitishwa

Fri, 9 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Katika ripoti hiyo ya CAG Charles Kichere, aliyoisoma jana bungeni jijini Dodoma, alisema TRA ilikuwa na changamoto mbalimbali katika ukusanyaji mapato.

“Katika ukaguzi wangu wa bidhaa zinazopita nchini kuelekea nchi jirani kupitia mipaka ya forodha ya Tunduma, Kasumulu, Rusumo, Kabanga, Mutukula, Namanga, Holili na Kigoma kwa kuangalia mfumo wa TANCIS na nyaraka za kusafirishia sikuthibitisha kuwa bidhaa zenye makadirio ya kodi ya forodha ya Sh. bilioni 5.14 zilitoka nchini,” alisema.

Ripoti hiyo pia imeeleza mafuta yaliyopitiliza muda nchini ambayo yalipaswa kwenda nchi jirani yenye ushuru wa forodha Sh. bilioni 12.14, yalibainika lita milioni 2.47 zenye makadirio ya ushuru wa forodha wa Sh. bilioni 1.97 yalibaki Tanzania bila kusafirishwa kwenda nchi zilizokusudiwa kwa muda uliopangwa wa siku 30.

Pia, lita milioni 14.08 za mafuta zenye ushuru wa forodha unaokadiriwa kufikia Sh. bilioni 10.43 zilizoshushwa ili kusafirishwa kwenda Zanzibar tangu mwezi Julai, 2019 hazijaondoshwa kwa muda uliopangwa wa siku 21.

“Kwa mujibu wa sheria ya forodha, mafuta yanayokaa nchini kwa zaidi ya muda uliopangwa yanapaswa kurasimishwa kwa matumizi ya ndani na hivyo kutozwa ushuru unaotakiwa,” alisema.

CAG katika ripoti hiyo alibainisha kodi zilizoshikiliwa na kesi zilizopo katika mamlaka za rufaa za kodi ni Sh. trilioni 360 na Dola za Marekani milioni 181.

“Nimebaini kuwa TRA imekuwa na kesi 1,097 za muda mrefu katika Mamlaka za Rufaa za Kodi zenye thamani ya Sh. trilioni 360 na Dola za Kimarekani milioni 181,” alisema.

Kadhalika, mwaka 2019/20, TRA ilikusanya Sh. trilioni 17.92 dhidi ya makisio yaliyowekwa ya Sh. trilioni 19.41, na kuwa na upungufu wa makusanyo kwa Sh. trilioni 1.49 sawa na asilimia nane ya jumla ya makisio ya makusanyo.

DENI LA SERIKALI

Deni la serikali hadi kufikia Juni 30, mwaka jana, lilikuwa Sh. trilioni 56.76 na la ndani lilikuwa Sh. trilioni 15.52, la nje Sh. trilioni 41.24, ikiwa ni ongezeko la Sh. trilioni 3.65 sawa na asilimia saba ikilinganishwa na deni la Sh. trilioni 53.11, lililoripotiwa mwaka wa fedha 2018/19.

Ongezeko hilo linajumuisha Sh. bilioni 652 za deni la ndani na Sh. trilioni tatu za deni la nje.

“Hadi Juni 30, mwaka 2020 deni la serikali lilikuwa linahimilika,” alisema.

Chanzo: ippmedia.com