Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil.1 zatengwa mafunzo kwa waongoza watalii

Kabuka.jpeg Fedha hizo zimetokana na mkopowa Tr.1.3 wa Uviko 19

Sat, 19 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO -19 imetenga shilingi bilioni 1.01 kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii wanawake takribani 1060 nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakati wa kuhitimisha mafunzo ya waongoza Watalii wanawake 89 yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

“Mafunzo haya ni mahususi kwa wanawake kama jitihada za makusudi kabisa za Serikali kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa za kuchangia katika maendeleo ya nchi kupitia utalii na kunufaika kupitia sekta hiyo” ” amefafanua Mhe. Masanja.

Amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri kwa kuitangaza vyema Tanzania ndani na nje ya nchi.

“Natambua mmekuwa mabalozi muhimu mnaotegemewa kuiuza nchi yetu hivyo sifa ya kwanza mnayotakiwa kuwa nayo ni uzalendo. Wageni mnaowapokea wana sifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa hivyo wakati mnatekeleza majukumu yenu mnapaswa kuwa na uelewa mpana wa shughuli za utalii na pia muwe na maadili, weledi na uadilifu”amesema Masanja.

Aidha, amewaasa waongoza watalii hao kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watalii wanapowasili nchini ili kujenga taswira nzuri ya Tanzania na kumfanya mtalii aweze kuru

Chanzo: www.tanzaniaweb.live