Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biharamulo kuzalisha tani 1,000 za kahawa

Kahawa Pc Biharamulo kuzalisha tani 1,000 za kahawa

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera inatarajia kuzalisha tani 1,000 za kahawa aina ya robusta sawa na kilo milioni moja ifikapo 2023.

Hayo yamebainika jana Machi Mosi, 2022 wakati mkuu wa wilaya hiyo Kemilembe Rwota alipokuwa akigawa miche bora ya kahawa aina ya robusta inayotoa matunda ndani ya mwaka mmoja na nusu hadi miaka miwili.

Ofisa kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamlo, Bruno Ngawagala amesema 2020/2021 wilaya hiyo ilizalisha tani 40 hadi 70 za kahawa ya maganda ambapo baada ya kugawa miche bora ya kahawa 5,000 wanatarajia kuzalisha tani 1,000 sawa na kilo milioni moja

"Kama halmashauri tuliwasilisha ombi bodi ya kahawa (TCB) kuomba kitalu cha kuotesha miche bora ya kahawa aina ya robusta laki tano (5) baada ya kuona mikahawa iliyopo mashambani imezeeka na matokeo ya maombi hayo ni hii miche tuliyogawa siku ya leo". Amesema Ngawagala

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Jjad Kagera famers ltdĀ  iliyozalisha miche hiyo katika kitalu cha Rukaragata kata ya Biharamulo mjini, Dk John Mbogoma amesema richa ya kampuni hiyo kupewa jukumu la kuzalisha miche 5,000 ya kahawa wamevuka lengo na kuzalisha miche 6,000.

Meneja wa bodi ya kahawa kanda ya Kagera, Melkiad Massawe ametaja lengo la kuzalisha miche hiyo kuwa ni kuwezesha wakulima wa kahawa kubadili miti ya zamani ipatayo 240 milioni iliyopo na kupanda miche bora ya kahawa na inayokinzana na magonjwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live