Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bidhaa za kilimo kukidhi soko la kimataifa

49676b8873961e5dfdd9bb7435414de5 Bidhaa za kilimo kukidhi soko la kimataifa

Tue, 30 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali inaendelea kuratibu mradi wa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya (MARKUP EU-EAC) unaolenga kuwezesha bidhaa za kilimo kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kukidhi viwango vya soko la Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stergomena Tax amesema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 bungeni mjini Dodoma leo (Mei 30, 2023).

Tax ameliambia Bunge kuwa bidhaa zilizopewa kipaumbele katika mradi huo ni kahawa, chai, parachichi, viungo na mbogamboga.

Mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Tanga, Morogoro, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe na visiwa vya Pemba na Unguja.

Mradi umewezesha wakulima kuzalisha mazao ya kilimo kwa kutumia mbegu bora na kuzingatia utunzaji wa mazingira, ambapo vyama vya ushirika 26 kutoka mikoa ya Njombe na Ruvuma vimepata hati za ubora na hivyo kukidhi vigezo vya kuuza mazao katika soko la Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live