Serikali imesema ziara ya Rais Dkt. Samia nchini China imesaidia bidhaa zaidi ya 8000 za Tanzania kuanza kuuzwa China bila kuwekewa ukomo wala ushuru.
"Kutoka mwaka 2018 January kwenye SADC tunapaswa kuuza bidhaa zetu bila ushuru wala kodi katika zile nchi 16 za SADC, tumepanua soko tumeenda Afrika nzima ambako nako tumelegeza masharti ya kuuziana "
Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ally Gugu katika Viwanja vya Sabasaba Dar es salaam wakati wa Mkutano wa Wadau wa Viwanda na Uzinduzi wa Mfumo wa Taarifa za Biashara (Biashara App).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Latifa Khamis amesema mfumo huo umezinduliwa ili kuwasaidia Wakulima na Watu wengine kupata taarifa ya bei za bidhaa “Tumeanza na Wakulima kwasababu Mkulima wakati mwingine anataka kuuza bidhaa na sisi tulio Mjini Wajanja tunaweza kumuendea shambani tukamdanganya bei kwamba Mjini kilo 500 kumbe Mjini bei kilo 2000 kwahiyo kupitia Biashara App Mkulima atajua bei na ataamua jinsi ya kuuza”