Mtaalamu wa epidemiolojia katika Wizara ya Afya, Dk Frenk Matulu amesema suala la takataka liko chini ya halmshauri, manispaa au jiji kwa sababu zina mifumo ya kuhakikisha taka zinapozalishwa zinapelekwa kutupwa kwa wakati bila kuleta madhara.
Amesema na wamekuwa wakihimiza suala hilo kusimamiwa lakini changamoto iliyopo ni kwamba wale waliopewa jukumu hilo hawafanyi kwa ufanisi na wakati mwingine wanatumia vifaa duni.
“Sisi kama Wizara ya Afya tumekuwa ni wasimamizi kuhakikisha taka zinapelekwa mapema maeneo maalumu ambayo yamepangwa, nielekeze kwa niaba ya wizara, wahusika wanaonasimamia taka wahakikishe zinasimamiwa vizuri na zinapelekwa maeneo husika kabla ya kuleta madhara kwa jamii,” amesema.