Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara ya nyama Arusha yasuasua, wafanyabiashara watoa sababu

89830 Nyama+pic Biashara ya nyama Arusha yasuasua, wafanyabiashara watoa sababu

Thu, 26 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Wafanyabiashara wa nyama katika Soko Kuu  jijini Arusha nchini Tanzania wamesema biashara zao zinakabiliwa na changamoto kutokana na wafanyabiashara kutoka nchi jirani ya Kenya kuruhusiwa kununua mifugo hai badala nyama jambo linaloongeza ugumu wa biashara yao.

Wakizungumza na Mwananchi leo Jumanne Desemba 24, 2019 mmoja wa wafanyabiashara hao, Daniel Lazaro amesema bei ya mifugo imepanda kutokana na mahitaji makubwa ya mifugo nchini Kenya na ushuru wanaolipa kwenye maeneo ya minada.

“Kipindi hiki biashara zetu sio nzuri idadi kubwa ya wateja wetu wamesafiri na kuna baada ya wateja ambao wamesimamisha oda zao unaona mwenyewe wateja wanakuja mmoja mmoja labda kesho wataongezeka,” amesema Lazaro

Naye Jonas Thomas amesema iwapo Serikali itaweka mfumo utakao wezesha ununuzi wa nyama badala ya mifugo hai kwa soko la Kenya utasaidia biashara yao kurudi katika hali ya kawaida kwa sababu wafanyabiashara wa Kenya wana mitaji mikubwa ukilinganisha na mitaji yao.

“Wafanyabiashara wa hapa Arusha hatuwezi kushindana kwenye bei na wenzetu kutoka Kenya wenyewe wananunua kwa bei iliyopo sokoni kwetu sisi inakua ngumu kumudu huo ushindani, Serikali iangilie kati kuinua biashara yetu,” amesema  Thomas

Kwa upande wake, Leon Shiyo amesema msimu wa sikukuu ya mwaka biashara yao haijawa nzuri ukilinganisha na miaka iliyopita  kutokana na wananchi kutokua na fedha za kufanya manunuzi akiamini huenda siku ya kesho inaweza kuwa nzuri kwao.

Mwaisumbe  amesema wafanyabiashara wa nyama katika mabucha wamekua wakitaka kupata faida kubwa bila kujali anachopata mfugaji na kwakua soko la biashara hiyo lipo huru ni vizuri kuwawezesha wafugaji kupata malipo yanayoendana na jasho lao.

Kuhusu kuwauzia nyama badala ya mifugo wafanyabiashara wa Kenya alisema hakuna sheria inayozuia ununuzi wa mifugo hai na ndio maana Serikali ikaweka soko la kimataifa la mifugo la Oriendeke ambalo lipo kilometa chache kutoka mpaka unaotenganisha Kenya na Tanzania .

“Longido tumeshaanza kutekeleza maagizo ya uchumi wa viwanda yupo mwekezaji ambaye amejenga kiwanda kikubwa kinatarajiwa kuanza uzalishaji Machi 2020 baada ya hapo utakua ni uamuzi wa mnunuzi kununua nyama au mifugo hai, Kenya wanategemea mifugo kutoka Tanzania kwa zaidi ya asilimia 90,” amesema Mwaisumbe

Chanzo: mwananchi.co.tz