Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara ya mahindi Tanzania na Kenya yazidi kushamiri

Mahindi.jfif Lori za mahindi Mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Kenya zimearifu kukua na kuongezeka kwa biashara ya uingizwaji wa mahindi nchini Kenya ambapo zimesema idadi ya mifuko ya mahindi inayoingia kenya imeongezeka kutoka mifuko 16,137 mwezi April kwa mwezi hadi mifuko 118,329 mwezi May baada ya kufikiwa kwa makubaliano mapya ya kuondoa vikwazo vya uingizaji wa mahindi kutoka Tanzania hadi Nairobi.

Mkuu wa wilaya ya Longido Bwa. Nurdin Babu amethibitisha taarifa hiyo iliyotolewa na Kenya na kuongeza kuwa, Tanzania na Watanzania kwa ujumla wamenufaika na fursa hiyo ya biashara kutokana na utaratibu unaotumika sasa wakuingiza mahindi Kenya ambapo ameshuhudia idadi kubwa ya lori zilizobeba nafaka kuingia nchini kenya. "Baada ya Rais wetu kuzuru Kenya, mambo yamebadirika sana, Wafanyabiashara kutoka Tanzania wamefurahishwa na maazimio yaliyofikiwa na Rais wa Kenya. Sisi wakazi wa longido ni mashahidi idadi kubwa za lori zinazovuka kusafirisha mahindi, ni fursa nzuri sana ya biashara" alisema Bwa.Babu.

Ameongeza kuwa pamoja na kwamba mahindi yanayoingia Kenya ni mengi lakini bado Tanzania ina akiba yakutosha ya chakula, na kuwatoa hofu wananchi yakukumbwa na baa la njaa.

Awali Wizara ya kilimo ya Kenya ilipiga marufuku uingizwaji wa mahindi nchini Kenya kwa madai kuwa mahindi kutoka Tanzania na Uganda yalikuwa na Sumu, Mgogoro ambao ulimalizwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada yakufanya ziara ya kikazi nchini Kenya na kuhutubia Bunge la Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live