Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara ya bidhaa bandia yaongezeka

EiCsk3VXcAA Y U 780x470 Biashara ya bidhaa bandia yaongezeka

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: Habarileo

Biashara ya bidhaa bandia nchini imeongezeka ukubwa kutoka nafasi ya tatu na kuwa ya pili, imeelezwa. Nafasi ya kwanza ya biashara haramu inashikwa na dawa za kulevya wakati zamani nafasi ya pili ilikuwa sukari za magendo, lakini sasa ni bidhaa za bandia.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio alieleza hali hiyo juzi wakati wa semina ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari iliyofanyika mkoani Dar es Salaam.

“Bidhaa bandia zina hasara nyingi kama kupoteza ajira, wawekezaji wanakimbia lakini hizi bidhaa kuongezeka kunachangiwa na wazalishaji wa bidhaa halisi kutoelimisha umma namna ya kutofautisha bidhaa halisi na bandia,” alisema Erio.

Alisema FCC imeendelea kufungua ofisi mpya kwenye kanda ili kupambana na bidhaa hizo bandia na hivi karibuni imefungua kwenda mikoa ya Mbeya, Mwanza na Arusha na hivyo kufanya ofisi hizo kufikia tano. Awali zilikuwapo Dar es Salaam na Dodoma.

Erio alisema vituo vya mpakani nchi nzima vipo vinane na juhudi zinaendelea kuviongeza. “Sasa hivi kwa mfano tupo kwenye mchakato wa kupata kituo kipya cha mpakani Kasumulo (Mpaka wa Tanzania na Malawi). Lengo tuwe na ofisi kwenye vituo vyote vya mpakani,” alifafanua.

Mkurugenzi Mkuu huyo alisema FCC itaweka maofisa wake kwenye njia zote za panya baina ya nchi na nchi kunakopita bidhaa bandia. “Njia za panya zipo nyingi sana mfano Sirari (Mpaka wa Tanzania na Kenya) kuna njia hizo 140, kuna mbunge aliwahi kusema Tunduma (Mpaka wa Tanzania na Zambia) kuna njia za panya 80,” alisema Erio

Chanzo: Habarileo