Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara ndogondogo zinachangia asilimia 40 pato la ndani Afrika

Biashara Ndogondogo Afrika Biashara ndogondogo zinachangia asilimia 40 pato la ndani Afrika

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

meelezwa kuwa, biashara ndogondogo ndizo zinazochangia asilimia 40 ya pato la taifa katika nchi za Afrika, lakini ndizo zinazokabiliwa na changamoto nyingi.

Hayo yameelezwa katiika Kongamano la Pili la Wafanyabiashara Wanawake Afrika chini ya mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (Afcta) linafanyika nchini Tanzania.

Kongamano hilo linafanyika huku ikielezwa kuwa, wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingii ikiwamo ukosefu wa mitaji na mikopo ya kuendeshea biashara.

Asilimia 90 ya biashara zote barani Afrika ni biashara ndogondogo na za kati na asilimia 60 kati ya hizo zinamilikiwa na wanawake. Hayo yameelezwa leo katika kongamano la wanawake chini ya eneo huru la biashara Afrika, linalofanyika jijini Dar es Salaam kwa mara ya pili sasa.

Ni katika mkutano huu unaofanyika chini ya wakfu wa mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (Afcta) ndipo wanawake wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wamekutana kujadili changamoto, fursa na mafanikio waliyoyapata katika mazingira ya biashara ndogondogo na za kati.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Kassim alikuwa ndiyo mgeni rasmi katika kongamano hilo na akaorodhosha changamoto kuu zinazowakabili wafanyabiashara wanawake ikiwamo ukosefu wa mikopo na mitaji yenye masharti nafuu, ukosefu wa taarifa sahihi na vikwazo katika biashara za mipakani.

Katibu Mkuu wa Afcta, Wamkele Mene kutoka Afrika Kusini, akatoa wito kuwa ni muhimu kuchukua hatua muhimu kwa kuondoa vikwazo vya kibiashara vinavyowakabili wanawake na vijana Afrika.

Kongamano hilo lililowajumuisha wafanyabiashara wanawake kutoka nchi zaidi ya 50 Afrika, viongozi wa ngazi za juu za serikali, mawaziri na makatibu wakuu kutoka nchi hizo, limejadili pia rasimu ya itifaki ya wanawake na vijana katika biashara inayotarajiwa kuanza kutumika Februari 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live