Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara mpya kusamehewa kodi kwa miezi 6 awali

62628 Wafanyabiasharapic

Thu, 13 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imependekeza kusamehe kodi mafanyabiashara au mwekezaji kwa kipindi cha miezi sita pindi anapopewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Msamaha huo, utaanza kutumika Julai Mosi 2019, ili kumuwezesha mfanyabiashara au mwekezaji kujiandaa na mahitaji yanayotakiwa katika shughuli anazofanya.

Vile vile kuondoa usumbufu, dhana ya woga wakati wa kuanza biashara ikiwamo mahitaji ya leseni ya biashara na vibali vingine.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phili Mpango wakati akiwasilisha makadirio na mapato ya Serikali kwa mwaka 2019/20.

Waziri Mpango amesema, “Hatua hii inatofautiana na hali ilivyo sasa ambapo mfanyabiashara anapopewa TIN anaanza kufanyiwa tathimi (tax assessment) ya mapato yake ya biashara na kutakiwa kulipa kodi.”

 

Habari zinazohusiana na hii



Chanzo: mwananchi.co.tz