Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki zabaini changamoto ukopeshaji viwanda

20894 Nmb+pic TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya NMB Plc imetaja sababu za benki za biashara kushindwa kutoa mikopo kwa miradi ya viwanda inayokadiriwa kuwa ya thamani ya Sh48 trilioni.

Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa serikalini, Filbert Mponzi amesema kiasi kikubwa cha fedha zinazokopeshwa na benki za ndani, zinakopeshwa kwa muda mfupi wakati miradi ya biashara inataka mikopo ya muda mrefu.

Amesemwa hayo leo usiku Oktoba 4, 2018  katika Jukwaa la Fikra la Mwananchi linalolenga kujadili fursa, changamoto na ufumbuzi kuelekea uchumi wa viwanda ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV.

Mponzi amesema utaalamu uliopo kwenye benki ni kwa ajili ya muda mfupi na imekuwa changamoto kwao kutathmini mikopo ya muda mrefu.

“Ni changamoto kubwa kwa benki nyingi kuchambua na kutathmini mikopo ya muda mrefu,” amesema Mponzi.

Mponzi amesema changamoto nyingine zinazokumba mikopo ya viwanda ni hatari zinazoambatana na miradi ya viwanda.

“NMB imekuwa ikifanya kazi na taasisi za fedha na Serikali kuhakikisha changamoto hizi zinazotokana na ukosefu wa utaalamu wa kuchambua mikopo ya viwanda,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz