Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ‘yakoshwa’ na ufanisi, ubunifu TSN

14897e42e4e1dae692af585b4aa58368 Benki ‘yakoshwa’ na ufanisi, ubunifu TSN

Fri, 25 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BENKI ya I&M imekoshwa na uwezo, ufanisi na ubunifu unaofanywa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya HabariLEO, HabariLEO Jumapili, Daily News, Sunday News na SpotiLeo katika kufikisha ujumbe kwa jamii.

Akizungumza jana katika Makao Makuu ya TSN Dar es Salaam wakati wa ziara ya uhusiano bora ya kazi kati ya benki hiyo na TSN, Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Anitha Pallangyo alibainisha kuwa TSN imekuwa mfano wa kuigwa kutokana na namna inavyochambua habari zake.

Akitolea mfano wa habari za biashara, alisema kuwa zimekuwa zikiandikwa kwa ufanisi kiasi cha kunufaisha wajasiriamali wengi huku akibainisha kuwa hata benki hiyo ni mnufaika wa habari za biashara za magazeti ya TSN.

Pia Anitha alizungumzia baadhi ya huduma zilizoongezwa na benki hiyo ambazo ni akaunti maalumu ya wanawake iitwayo ‘tunaweza’yenye nia ya kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi ambapo hawakatwi fedha za kila mwezi za akaunti na huduma za kutunza fedha za vikundi.

Alisema benki hiyo yenye makao makuu nchini Kenya pia inapatikana Rwanda na Mauritius huku hapa nchini inayo matawi Dar es Salaam, Moshi na Mwanza.

Kwa upande wake, Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Januarius Maganga alisema mbali na kuchapisha magazeti, kampuni hiyo ina huduma za habari mtandaoni zinazosanifiwa na waandishi mahiri.

Alisema: “Kama kampuni ikinunua magazeti yetu mtandaoni, kuna punguzo kubwa la bei huku huduma zake zikiwafikia wateja sahihi na kwa uharaka zaidi. Pia TSN ina kiwanda kinachapisha bidhaa kama magazeti, majarida, kalenda na huduma nyingine nyingi za uchapishaji.”

Chanzo: habarileo.co.tz