Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya UBA sasa yaunganishwa GePG

Debit MasterCard1.png Benki ya UBA sasa yaunganishwa GePG

Thu, 9 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imeiunganisha Benki ya UBA kwenye mfumo wa malipo wa serikali wa kielektroniki (GePG) ili kuwasaidia Watanzania waweze kulipa kodi kwenda taasisi zaidi ya 600 kwa haraka zaidi.

Mkuu wa kitengo cha sekta ya umma wa benki hiyo, Dominick Timothy, alisema na kueleza kuwa kwa sasa watu wataweza kulipa kwa haraka malipo ya kodi na yasiyo ya kodi kupitia UBA.

Alisema benki hiyo imepata kibali cha kuwa moja kati ya benki nane nchini zinazofanya malipo ya kodi na yasiyo ya kodi kwenda kwa taasisi za serikali kupitia mfumo wa GePG.

Timothy alisema kuwa kuunganishwa kwa benki yake katika mfumo wa GePG ni moja wapo ya njia za taasisi hiyo ya fedha kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na serikali chini ya Rais John Magufuli.

“Kutokana na benki yetu kuunganishwa na mfumo wa GePG itaoanisha mfumo huu na njia zake za kidijitali za kibenki ambazo ni kupata huduma kwa njia ya simu, mtandao na zile za Leo Chatbot, USSD Magic Banking na Webcollect,” alisema.

Alisema lengo la kuunganisha na njia hizo za kibenki ni ili kuwawezesha Watanzania kufanya malipo ya serikali popote pale walipo pasipo kulazimishwa kwenda katika tawi la benki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live