Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya PBZ kufunga ATM 14 Z’bar, Dar

63225 Pic+pbz

Tue, 18 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) inatarajia kufunga mashine za ATM (14) katika maeneo mbalimbali Zanzibar na Tanzania Bara kwa kipindi cha mwaka 2019/20 ya Sh389.56 bilioni ili kuongeza  ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa amebainisha hayo leo Jumanne Juni 18, 2019 katika mkutano wa baraza la wawakilishi wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa wizara yake kwa mwaka 2019/20.

Amesema lengo kuu la kufunga mashine hizo ni kuona huduma za benki zinapatikana kwa ukaribu hasa kwa wale wateja walio mbali na maeneo yanayopatikana mashine hizo Zanzibar na Tanzania bara.

Waziri huyo ameyataja maeneo yatakayofungwa mashine hizo ni Gombani, Mtambile, Wete kwa upande wa Pemba na upande wa Unguja ni Amani, Mwamchina na Mwera na Dar es Salaam mashine zitafungwa mtaa wa Tandika pamoja na Kigamboni.

Hata hivyo, Balozi Ramia amesema katika hatua nyengine benki hiyo inatarajiwa kuimarisha mfumo mpya wa kibenki ili kubaini dosari na kurekebisha, kuanza kutoa huduma za kadi za kimataifa (Visa na Master Card), kutoka huduma za kibenki kwa kutumia mawakala.

Amesema kuweka mfumo wa kupima utendaji wa wafanyakazi, kuanza na kukamilisha ujenzi wa tawi pacha la Malindi, kuanza ujenzi wa makao makuu ya benki hiyo Mazizini nje kidogo ya mji wa Unguja ambapo katika shughuli hizo benki hiyo inatarajia kutumia Sh30.65 bilioni kwa matumizi ya kawaida na Sh21.00 bilioni kwa kazi za maendeleo.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz