Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya NBC Yakabidhi Vifaa Tiba kwa Ajili ya Kliniki Inayotembea

NBC ZANZIBAR 1 1?fit=700%2C467&ssl=1 Benki ya NBC Yakabidhi Vifaa Tiba kwa Ajili ya Kliniki Inayotembea

Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Benki ya NBC Yakabidhi Vifaa Tiba kwa Ajili ya Kliniki Inayotembea August 30, 2021 by Global Publishers

Waziriwa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, AhmedNassor Mazrui (wa pili kushoto) akipokea moja ya vifaa vifaa tiba vitakavyotumikakwenye kliniki inayotembea (Mobile clinic) kutoka kwa maofisa waandamizi wabenki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Bw ElibarikiMasuke  (wa pili kulia)wakati wa haflahiyo iliyofanyika ofisini kwa waziri huyo, Zanzibar. Vifaa hivyo vimetolewabenki hiyo kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afyahususani ya mama na mtoto visiwani humo.

Zanzibar:Agosti 27, 2021:Benki ya Taifa ya Biashara NBC, hii leo imekabidhi msaada wa vifaa tiba ikiwemoUtraSound machine vitakavyotumika kwenye kliniki inayotembea (Mobile clinic)ambayo pia imetolewa na benki hiyo kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo.

Akizungumzamara baada ya kupokea  vifaa hiyo vyenyethamani ya zaidi ya Sh mil 19.5 Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui pamoja na kuishukurubenki hiyo kwa msaada huo, alisema serikali hiyo itahakikisha msaada huoutatumika kama ilivyokusudiwa.

Waziriwa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, AhmedNassor Mazrui (alieketi) akizungumza na maofisa waandamizi wa benki ya NBCwakiongozwa na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Bw ElibarikiMasuke  (kushoto) wakati wa makabidhianoya vifaa hiyo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo Zanzibar. Wengine ni pamojana  Meneja wa benki ya NBC tawi laZanzibar Bw Ramadhani Lesso (Kulia) na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kiislam waBenki hiyo Mohamed Nuh

“Msaadahuu ni muhimu na kiukweli unahitajika sana. Jukumu letu kama serikali nikuhakikisha vifaa hivi vinatunzwa na vinatumika kama ilivyokusudiwa ili viletetija iliyolengwa kwa maana visaidie haswa kuokoa maisha ya wazanzibar wakiwemowakina mama na watoto hasa walipo pembezoni.

Aliahidikwa niaba ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendeleza ushirikiano na benkihiyo hususani kwenye masuala mbalimbali ikiwemo yale yanayohusu ustawi wa jamiihuku akibainisha kuwa uimara wa benki hiyo kwenye utoaji wa huduma zakevisiwani humo kwa kiasi kikubwa unachagizwa na namna inavyoshirikiana na jamiiya Wazanzibar ikiwemo kibiashara na mambo ya kijamii.

“Naaminikabisa uimara wa benki ya NBC tangu ilipoanza kutoa huduma zake hapa Zanzibarni matokeo ya ushirikiano iliyonayo na jamii ya Wazanzibar…nawapongeza sana naninaomba muendelee kuguswa zaidi,’’ aliongezea.

Mkurugenziwa wateja binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke  akisaini kitabu cha wageni alipoingia kwenyeofisi ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na WatotoZazibar, Ahmed Nassor Mazrui wakati wa makabidhiano hayo.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki ya NBC Bw ElibarikiMasuke alisema pamoja na msaada huo benki hiyo itaendelea kuhudumia vifaa hivyohata pale vitakapokuwa vinapata hitirafu za kiufundi.

“Benkiya NBC tumekuwa tukiguswa na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye huduma zaafya hapa nchini ikiwemo Zanzibar na ndio maana tumekuwa mstari wa mbelekuhakikisha tunashirikiana na serikali zote mbili kukabiliana na changamotozinazohusu sekta hii muhimu.’’

“Tunaaminikupitia vifaa hivi vitakavyofungwa ndani ya kliniki inayojongea wataalamu waafya wataweza kuwafikia walengwa popote walipo hususani wale waliopo pembezoniwakiwemo wakina mama na watoto na kupitia msaada wa Mungu tutaweza kuokoamaisha yao,’’ aliongeza.

Mkurugenziwa wateja binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (kulia) akisalimianana   Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui wakati wa makabidhianohayo.

Akizungumziamsaada huo Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto, Wizara ya Afya ZanzibarBi Wanu Bakari alisema msaada huo umefika wakati muafaka wakati serikali hiyo ikipambanakusogeza huduma za afya hususani maeneo ya pembezoni ili kuepukana nachangamoto ya vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua.

“Tunaishukurusana benki ya NBC kwa kuliona hili na kwa kweli wametugusa sana! Kwa mfanokupitia kliniki hii tutaweza kutoa  hudumaya Utrasound ambapo kwa kwasasa tunakabiliwa na uhaba wa huduma hii hivyotatizo linakwenda kupungua. Zaidi pia miongoni mwa vifaa hivi pia vipo vifaavya uchunguzi wa afya za kina mama wajawazito kitu ambacho kitatusaidiakuwafanyia uchunguzi kwa haraa pale itakapohitajika kabla hawajapata madharazaidi,’’ aliongezea.

Menejawa benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw Ramadhani Lesso (Kulia) akisalimiana na   Waziri waAfya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, AhmedNassor Mazrui wakati wa makabidhiano hayo.

“Tunaaminikupitia vifaa hivi vitakavyofungwa ndani ya kliniki inayojongea wataalamu waafya wataweza kuwafikia walengwa popote walipo hususani wale waliopo pembezoniwakiwemo wakina mama na watoto na kupitia msaada wa Mungu tutaweza kuokoamaisha yao,’’ aliongeza.

Akizungumziamsaada huo Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto, Wizara ya Afya ZanzibarBi Wanu Bakari alisema msaada huo umefika wakati muafaka wakati serikali hiyo ikipambanakusogeza huduma za afya hususani maeneo ya pembezoni ili kuepukana nachangamoto ya vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua.

“Tunaishukurusana benki ya NBC kwa kuliona hili na kwa kweli wametugusa sana! Kwa mfanokupitia kliniki hii tutaweza kutoa  hudumaya Utrasound ambapo kwa kwasasa tunakabiliwa na uhaba wa huduma hii hivyotatizo linakwenda kupungua. Zaidi pia miongoni mwa vifaa hivi pia vipo vifaavya uchunguzi wa afya za kina mama wajawazito kitu ambacho kitatusaidiakuwafanyia uchunguzi kwa haraa pale itakapohitajika kabla hawajapata madharazaidi,’’ aliongezea.

Chanzo: globalpublishers.co.tz