Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Mwanga Hakika yawa mkombozi wilayani Mwanga

Mwangani Mwenyekiti wa Bodi ya Benki akimkabidhi DC na DAS msaada wa madawati

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Mwanga Hakika Bank imetoa jumla ya madawati na meza 472 yenye thamani ya zaidi ya milioni 30 kwa shule za sekondari Wilayani Mwanga ili kukabiliana na uhaba wa madawati wilyani humo.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi 30,000,000 vitasaidia kupunguza uhaba wa viti na meza kwa wanafunzi wapatao 13,429 kutokana na ongezeko la wanafunzi 233 kwa mwaka wa masomo 2021/2022.

Kabla ya msaada huo, Wilaya hiyo ilikuwa na upungufu wa viti na meza 689 kwenye shule 10 kati ya 26 za Sekondari Wilayani humo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Mwanga Hakika, Mhandisi Ridhuan Mringo alisema lengo la msaada huo ni kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora ya kujifunzia.

“Benki yetu inatekeleza sera yake ya wajibu kwa jamii kwa kuangalia maeneo yenye uhitaji ikiwamo sekta ya elimu.Msaada huu wa madawati ni katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia Pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukuza sekta ya elimu hapa nchini,” alisema Mringo.

Alisema benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo ili kuhakikisha malengo makubwa ya Taifa yanafikiwa kwa asilimia kubwa.

“Benki yetu imeweza kukua kutoka kuwa benki ndogo na kuwa benki inayokuwa kwa kasi.Tunaamini ukuaji wa benki hii unatupa uwezo wa kuweza kuchangia zaidi kwenye masuala ya kijamii kama ilivyofanyika hii leo,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Abdallah Mwaipaya aliishukuru Benki ya Mwanga kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo Wilayani hapo na kwamba itasaidia kufanikisha mipango mikubwa ambayo Wilaya hiyo imejiwekea kwa mwaka 2021/2022.

“Madawati haya yanakwenda kwenye shule ambazo tulikuwa tuna upungufu mkubwa wa madawati zaidi ya 600.Kwa ujumla tunashukuru kwa madawati haya yatakwenda kumaliza matatizo ya madawati kwenye shule za sekondari na baadaye tutageukia shule za msingi,” alisema.

Mbali na msaada huo, Wilaya hiyo imefanikiwa kujenga madarasa 50 katika shule za Sekondari ikitumia Shilingi 976,000,000 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ikiwamo bajeti kuu Shilingi 500,000,000 fedha za UVIKO-19 200,000,000, Fedha za ndani 30,000,000 pamoja na fedha za EP4R Shilingi 237,000,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live