Dar es Salaam.Uongozi wa Benki ya Exim Tanzania umezindua kampeni inayolenga kuhamasisha wateja kuhusu matumizi ya mtiririko wa huduma maalumu za kiusalama katika masuala ya fedha zinazotolewa na benki hiyo.
Mtiririko huo utasaidia wateja kupata huduma mbalimbali ikiwamo ya usafirishaji wa fedha kwa usalama, malipo ya huduma za kisasa za hundi pamoja na huduma ya kuweka fedha kwenye akaunti ya benki hiyo.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu Septemba 16,2019.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa benki hiyo Stanley Kafu amesema kupitia huduma hizo wateja whawatahitaji kupanga foleni kwenye matawi ya benki hiyo kwa ajili ya kupata huduma za kifedha.
“Huduma hizi ni sehemu ya mkakati wa benki ya Exim Tanzania kutoa huduma kwa wateja bila kubanwa na muda wa kazi au umbali wa kijiografia,”amesema Kafu.
Akizungumzia huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama Kafu amesema ina lengo la kumuondolea mteja hatari ya kuibiwa, kuvamiwa, kunyang’anywa fedha wakati wa kuzitoa ofisini kwake kupeleka benki.
Pia Soma
- Wafanyakazi wa Serikali wafurika kuomba kustaafu kwa hiari
- Magufuli ampa agizo Makonda kuhusu miradi ya Coco Beach
- Sadc yajidhatiti kufikia soko la pamoja kupitia sekta ya miundombinu na uchukuzi
“Huduma hii ni kwa wateja ambao wanatoa na kupokea hundi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali kama vile vyuo vikuu, shule, viwanda, kampuni za usafirishaji na biashara za mitandao,” amesema Kafu.
Kuhusu huduma za hundi, Kafu amesema huduma hiyo inayotumia ‘scanner’ itamwezesha mteja kuweka hundi zake wakati wowote bila kutembelea tawi lolote la benki.
“Hakuna haja ya kupanga foleni tena, huduma ipo ofisini au nyumbani kwako. Huduma hii ni maalumu kwa wateja wote wenye biashara ambazo zinapokea hundi kwa wingi kila siku bila kujali kiasi gani cha fedha za Kitanzania au dola za Marekani,” amesema Kafu.