Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Exim yateua vigogo watatu

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya Exim Tanzania imetangaza uteuzi wa ofisa mtendaji mkuu mpya na maofisa wengine wawili wa nafasi za juu ambazo ni mkuu wa operesheni (COO) na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu Mei 6, 2019 na bodi ya benki hiyo inaonyesha kuwa Jafferi Matundu ndiye aliyeteuliwa kuiongoza benki hiyo ambayo jumla ya mali zake ni zaidi ya Sh1 trilioni ikiwa na kampuni kanzu Tanzania na Commoro.

“Uteuzi wake kama ofisa mtendaji mkuu wa benki unaonyesha imani ya watu waliyonayo juu yake katika kuiletea maendeleo zaidi benki yetu,” inaeleza taarifa hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Matundu ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha na uongozi alikuwa akikaimu nafasi hiyo takriban mwaka mmoja sasa.

Matundu kwa miongo kadhaa amekuwa akifanya kazi katika taasisi za ukaguzi wa fedha kwa benki za biashara, shahada yake ya kwanza ya fedha aliichukulia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na shahada ya uzamili ya uongozi aliichukulia Chuo cha Oxford, Marekani.

Kadhalika bodi imemteua David Lusala kuwa mkuu wa operesheni, kabla alikuwa mkuu wa kitengo cha tahadhari (risk) na kaimu mkuu wa kitengo cha teknolojia kwa zaidi ya mwaka.

Kwa uteuzi huo mpya, Lusala atawajibika kuiongoza benki katika mapinduzi ya kidijitali, ubunifu na shughuli nzima za uendeshaji kwa ujumla.

Lusala ana uzoefu wa miaka 12 katika masuala ya fedha na teknolojia akiwa na shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara kutoka Chuo Kikuu cha Wales, Uingereza.

Pia, bodi hiyo imemteua Kalpesh kama mjumbe huru wa bodi sambamba na taarifa ya kukaribia kustaafu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa hiyo, Said Mwema.



Chanzo: mwananchi.co.tz