Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Dunia yakanusha Uganda kuingia Uchumi wa Kati

Museveni Uchumi Rais Museveni

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Dunia imesema pato la kila mwananchi wa Uganda ni dola 850 kwa mwaka wa fedha unaoishia 2022, huku uchumi ukikua kwa wastani wa asilimia 3.7 ambapo ni chini sana ya kiwango cha chini cha kipato cha kati cha dola 1,045 ambacho kilielezwa na Rais Yoweri Museveni katika Hotuba yake kwa Taifa mnamo Juni 7.

Katika hotuba hiyo, Rais Museveni alibainisha licha ya #COVID19 na mfumuko wa bei duniani uchumi ulikua na kuingia kiwango cha kati, hata hivyo Benki ya Dunia ilikadiria kuwa licha ya ukuaji wa uchumi, idadi ya watu pia iliongezeka kwa takriban kiwango sawa, na kuacha pato la kila mtu palepale.

Katika kupima madaraja ya mapato ya nchi, Benki ya Dunia hutumia Pato la Taifa, ambalo linajumuisha mapato yanayopatikana kwa wakazi wa ndani na nje ya nchi na kugawanywa na idadi ya Raia wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live