Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Dunia: Uchumi wa Iran Ulikua zaidi 2021

Uchumi Iran Mafuta Iran

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Dunia imesema uchumi wa Iran ulistawi kwa asilimia 3.1 mwaka 2021 na hivyo kupiga hatua zaidi ya utabiri wa benki hiyo ambayo ilikuwa imetabiri Juni mwaka jana kuwa ustawi huo ungekuwa kwa asilimia moja.

Taarifa ya Benki hiyo iliyotolewa hapo jana (Jumapili) kuhusu 'Makadirio ya Ustawi wa Uchumi wa Dunia' inaonyesha kuwa Jumla ya Pato la Taifa (GDP) la Iran lilifika asilimia 3.1 mwaka 2021 na hivyo uchumi wa nchi hio umeweza kustawi kwa kasi zaidi ya ilivyotabiriwa.

Aidha jumla ya pato la taifa la Iran kwa mwaka 2020 lilikuwa ni 3.4 baada ya uchumi kudorora kwa asilimia 6.8 mwaka 2019 kutokana na vikwazo mbalimbali vya kiuchumi vilivilivyowekewa taifa hilo na mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani ambavyo vilizuia nchi hio kuuza nje mafuta ghafi ya petroli.

Ustawi wa uchumi wa Iran kwa muda wa miaka miwili mfululizo unajiri pamoja na kuwa Marekani iliimarisha vikwazo vyake mwaka jana wakati nchi hio ikiwa katikati ya vita dhidi ya maambukizi ya COVID-19.

Tawkimu za Benki ya Dunia zinathibitisha ukweli katika kauli ya wakuu wa Iran ambao wanasema kuwa nchi hio imeweza kuvuka athari mbaya za vikwazo vya Marekani na janga la COVID-19.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mwaka 2021 GPD ya Iran ilikuwa juu zaidi ya Saudi Arabia ambayo ni mshirika mkubwa wa Marekani. Benki hiyo imebaini kuwa GDP ya Saudi Arabia, muuzaji mkubwa zaidi ya mafuta duniani, ilikua kwa asilimia 2.4 kwa mwaka huo huo.

Ripoti imetabiri kuwa, katika mwaka huu wa 2022, uchumi wa Iran utakua kwa asilimia 2.4

Chanzo: www.tanzaniaweb.live