Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Credit Suisse kutoa mkopo wa Sh450 bil

11626 Benki+pic TanzaniaWeb

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya Credit Suisse ya nchini Uingereza imeonesha nia ya kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya Dola 200 milioni za Marekani (Sh450 bilioni).

Fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwamo ya umeme na reli.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha Wizara ya Fedha na Mipango jana, inaeleza kuwa hayo yamebainishwa katika mkutano kati ya waziri wa wizara hiyo, Dk Philip Mpango na ujumbe wa benki hiyo ukiongozwa na mkurugenzi wake mkuu, Lawrence Fletcher.

Dk Mpango alisema tayari zipo hatua mbalimbali zimefikiwa katika kufanikisha upatikanaji mkopo huo katika mwaka wa fedha wa 2018/19.

Aliitaja miradi mingine ambayo Serikali ina mpango wa kuitekeleza kuwa ni ujenzi wa bwawa la umeme la Rufiji (Rufiji Haydro Project), ambalo kukamilika kwake kutasaidia kuzalisha megawati 2100 utakaotumika kuchochea uchumi wa viwanda.

Dk Mpango alibainisha kuwa Serikali inatekeleza miradi ya kupanua bandari za Dar es Salaam, Tanga na Kigoma na ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara ambazo licha ya kuhudumia Tanzania, nchi jirani ya Rwanda na Burundi pia zitanufaika.

Naye Fletcher alisema benki hiyo inaangalia uwezekano wa kufadhili miradi ya kipaumbele ya Serikali ili kuweza kufanikisha nia yake ya kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Fletcher alisema watatoa mkopo huo baada ya hatua kukamilika katika mwaka huu wa fedha ili kuweza kufanikisha kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano kati ya beki hiyo na Tanzania.

Chanzo: mwananchi.co.tz