Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Benki punguzeni riba watu wakope’

Uchumi Kupanda ‘Benki punguzeni riba watu wakope’

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa amezitaka benki mbalimbali nchini kupunguza riba, ili kutoa fursa kwa wateja kukopa na kufanya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali.

Mtahengerwa ametoa rai hiyo jijini Arusha katika mkutano wa wadau wa Benki ya Maendeleo (TIB), Kanda ya Arusha na kusisitiza kuwa endapo benki zikipunguza riba katika mikopo, Watanzania wengi wataweza kukopa na kufanya uwekezaji wenye tija utakaoinua uchumi wa nchi, badala ya wawekezaji wa nje kuja nchini kuwekeza.

“Benki punguzeni riba ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuwekeza zaidi nchini, ikiwemo badala ya kutegemea wawekezaji kutoka nje ya nchi pekee waje kuwekeza nchini, tunataka Watanzania wawekeze kupitia benki na kuwa mamilionea kutoka nchini,” amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB,Lilian Mbassy amesema katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma, benki hiyo imekutana na wateja hao kutokana na kutambua umuhimu wa sekta binafsi katika shughuli za kiuchumi nchini.

Wakati huo huo,mmoja kati ya mtumiaji wa benki hiyo, Wilfred Mberesero ambaye ni Mkurugenzi wa Mberesero Lodge &Tent Camps, alisema benki hiyo ni nzuri kwani inatoa muda mrefu wa mikopo ya uwekezaji na ni benki mojawapo inayotoa muda mrefu wa urejeshwaji wa mikopo na kutoa rai kwa Watanzania mbalimbali kutumia benki hiyo kwa ajili ya kufungua fursa za kibiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live