Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki kuwakopesha machinga bila dhamana

Kitok Ed.jpeg Benki kuwakopesha machinga bila dhamana

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mkurugenzi Mwendeshaji wa benki hiyo, Esther Kitoka, alibainisha mpango huo wakati akizungumza kwenye semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa viongozi wa wafanyabiashara wa chakula kwenye masoko ya Dar es Salaam na Pwani.

Alisema benki nyingi zimekuwa zikiwalenga zaidi watu wakubwa na kusahau wafanyabiashara wadogo na ndiyo sababu benki hiyo imeamua kuanzisha huduma hiyo ili wakopeshwe na kukuza mitaji yao.

“Tumeona kundi hili limesahaulika ndiyo sababu tumeona tutengeneze bidhaa ambayo itawarahisishia wafanyabiashara hawa ili tuwape unafuu wa kifedha ndiyo sababu tumewaita hapa kuwaelezea bidhaa hiyo mpya,” alisema.

Alisema benki hiyo inaamini kundi hilo ni muhimu sana na likiinuliwa kwa kupewa mikopo linaweza kukua na kufanyabiashara kubwa zitakazowaingizia kipato hivyo kukuza kipato cha familia na taifa kupitia kodi mbalimbali.

Naye Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Isabela Maganga, alisema waliamua kuanzisha bidhaa hiyo baada ya kundi hilo kushindwa kupata mikopo kutokana na masharti magumu ya kupata mikopo ikiwamo kulazimika kuwa na dhamana.

Alisema Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na masoko zaidi ya 45, hivyo benki hiyo itajitahidi kuwafikia na kuwapa elimu kuhusu bidhaa hiyo ili wale wanaotaka mikopo waweze kukopa kupitia vikundi.

“Masoko ni sehemu muhimu sana ambako Watanzania wengi wanafika kupata mahitaji mbalimbali, ndiyo sababu tumeona umuhimu wa kuwaita kuwaelimisha kuhusu bidhaa hii.”

Mmoja wa wafanyabiashara wa Soko la Feri, Mwasi Abdalah, alisema huduma iliyoanzishwa na benki hiyo itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wengi wadogo ambao hawawezi kukopa benki.

Alisema wafanyabiashara wanashindwa kukua kutokana na mitaji yao kuwa midogo na wanashindwa kukopa ili kukua kutokana na masharti magumu kwenye taasisi za fedha.

Chanzo: ippmedia.com