Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki Standard Chartered Tanzania yazindua huduma nyingine mpya

70243 Benki+pic

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya Standard Chartered imezindua huduma ya mashine za kuwekea fedha (CDM) kwa wateja wake wakubwa na wa kati ili kuwaondolea usumbufu wa gharama na muda pindi wanapotaka kuhifadhi fedha katika akaunti zao.

Mashine hizo zenye uwezo wa kuhifadhi noti 10,000 zitawekwa kwa wateja wao nchini nzima wenye mauzo ya fedha taslimu nyingi ambao hulazimika kwenda benki kuhifadhi fedha hizo mara kwa mara, tayari kuna mashine saba zinafanya kazi kwa wateja tofauti.

Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 6, 2019 jijini Dar es Salaam na Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wa kati wa benki hiyo,  James Meitaron, amesema hilo litakuwa tawi dogo na mashine hiyo ina uwezo wa kuhesabu fedha yenyewe na kuzichambua feki na halisi sanjari na kutoa ripoti ya kiasi kilichoingizwa.

“Wateja tunaowalenga hapa ni wauzaji wa vinywaji, vituo vya mafuta, maduka makubwa na wengine wanauza fedha tasilimu nyingi kwa siku, mashine zina usalama wa hali ya juu na pindi mteja wanapoweka fedha zinaingia moja kwa moja kwenye akaunti yake na atapatiwa risiti,” amesema James Meitaron.

Amesema suala la usalama wa fedha na mashine hiyo litakuwa ni jukumu la benki, Standard Chertered itakuwa inazisafirisha fedha hizo pindi zinapojaa kuwa kuzipeleka katika matawi yake.

Chanzo: mwananchi.co.tz