Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki M yawekwa chini ya usimamizi wa BoT

9713 Bot+pic TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kutokana na upungufu wa ukwasi Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imechukua usimamizi wa Benki M Tanzania kuanzia leo, Agosti 2.

Akiongea na waandishi wa habari, Gavana wa BoT Profesa Frolens Luoga amesema uamuzi huo umetokana na benki hiyo kuwa na ukwasi mdogo kuliko matakwa ya Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

"Upungufu wa ukwasi ulioshuhudiwa katika benki hii unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa Benki M kunahatarisha amana za wateja wake hivyo kwa siku 90 kuanzia sasa benki hiyo haitatoa huduma," amesema Profesa Luoga.

Ameongeza kuwa BoT imeisimamisha bodi ya wakurugenzi na uongozi wa Benki M na mamlaka hiyo ya juu ya usimamizi wa sekta ya fedha itakuwa ikifanya tathimini ya kusaidia kupata ufumbuzi wa suala hilo.

Benki M inakuwa ya 10 kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa BoT ndani ya miaka miwili.

Benki sita kati ya zilizowekwa chini ya uangalizi zimefutiwa leseni za biashara na tatu zikiunganishwa na nyingine.

Kati ya zilizofutiwa leseni ni Benki ya FBME na Benki ya Wananchi Mbinga wakati Twiga Bancorp na Benki ya Wanawake (TWB) zikiunganishwa na Benki ya Posta na Benki ya Wananchi Tandahimba ikiungana na CRDB.

Chanzo: mwananchi.co.tz