Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki Kuu Tanzania yataja maeneo ya kubadilishia fedha Arusha

28671 Benki+pic TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema huduma ya kubadilisha fedha jijini Arusha inapatikana katika benki za biashara na hoteli za kitalii.

Novemba 19, 2018 BoT kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliendesha operesheni kwenye maduka ya kubadilishia fedha na kubaini ukiukwaji wa sheria na utaratibu wa biashara.

Ilibaini maduka mengi kutokidhi vigezo hivyo kutakiwa kurejesha leseni na kufunga biashara zao.

Tangu kufanyika kwa operesheni hiyo hadi leo mchana Jumamosi Novemba 24, 2018 huduma katika maduka hayo hazijarejea kama awali.

Leo, naibu gavana wa BoT, Dk Bernard Kibesse amesema huduma ya kubadilisha fedha zinapatikana kwenye benki za biashara, maduka ya kubadilishia fedha na hoteli za kitalii kote nchini kwa mujibu wa sheria za nchi.

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa huduma za kubadilisha fedha za kigeni jijini Arusha zinapatikana kwenye hoteli za kitalii na benki za biashara kwa mujibu wa sheria na kanuni za Benki Kuu ya Tanzania, " amesema Dk Kibesse.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz