Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Benk ya Kilimo ipunguze riba’

Kilimo ‘Benk ya Kilimo ipunguze riba’

Tue, 12 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imeagiza Benki ya Kilimo nchini kuhakikisha inashusha riba kutoka asilimia 11 hadi 9 kwa mkulima wa kahawa kupitia vyama vya Chama Kikuu cha ushirika Kagera(KCU) na Chama Kikuu cha Ushirika Karagwe na Kyerwa(KDCU).

Aidha, imesema haizuii sekta binafsi kununua kahawa isipokuwa imewakataza kununua kwa mkulima moja kwa moja.

?Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, alipokuwa akizungumza na viongozi kutoka mikoa inayolima zao la Kahawa hapa nchini.??

Bashe alisema lengo la kuitaka benki hiyo ishushe riba ni kuwasaidia wakulima kuendesha kilimo hicho.

?Alisema wakulima hao wamekuwa wakipata hasara kwenye kilimo hicho, hivyo serikali inataka wanufaike na zao hilo la kibiashara.

?"Ninaomba kikao hiki kiwe suluhisho la wakulima wa kahawa mnatakiwa kujadili kwa umakini na kutoka na kitu kimoja,ili kujenga ushirika wa haki ambao utamlinda mkulima,” alisema Bashe.

?Kuhusu ununuzi wa zao hilo, Bashe alisema sekta binafsi inapaswa kununua katika vyama na si kwenda kwa wakulima mmoja mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live