Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Belmont Hotel kukamuliwa Bilioni 1 na NSSF.

Delmont Hotel Belmont Fairmount Hotel Limited

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama imeamuru Hotel ya Belmont Fairmount Hotel Limited iliyopo jijini mwanza imetakiwa kulipa Mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF shilingi Bilioni 1 kama Kodi ya Pango.

Hili ni pigo lingine kwa Hotel hiyo Maarufu jijini Mwanza ambapo mwezi Octoba mwaka 2019 iliondolewa kwenye jengo la NSSF kwa kushindwa kulipa kodi ya pango.

Hotel hiyo ilitakiwa kulipa bilioni 1.5 kama pango ya miaka 5 tangu octobar mwaka 2016 lakini tangu hapo imelipia kiasi cha shilingi milioni 600.

Kabla ya NSSF kulichukua jengo hilo, Belmont Hotel ilipewa notisi ya miezi miwili kuwasilisha malipo. Ambapo pia Notisi hiyo ilipunguza gharama ya pango kutoka milioni 600 kwa mwezi hadi milioni 45 kwa mwezi.

Akijitetea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hotel hiyo Bw. Philemon Tei ameiambia mahakama kuwa aliilipa NSSF milioni 600 wakati ambao ameshitakiwana na kwamba madai ya kushitakiwa kulipa milioni 900 kama kodi ya pango sio ya kweli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live