Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei za nyama, maziwa na pombe kupanda Afrika Mashariki

Pombe, Maziwa Bei za nyama, maziwa na pombe kupanda Afrika Mashariki

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: BBC

Uagizaji bidhaa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) sasa utavutia ushuru wa juu zaidi wa asilimia 35 baada ya mataifa yote washirika kulipa ushuru wa Pamoja wa Nje (CET) kwa bidhaa za bendi ya nne.

Bidhaa katika bendi hii ni pamoja na bidhaa za maziwa, nyama, nafaka, pamba, nguo, chuma na mafuta ya kula na vileo.

Nyingine ni samani, bidhaa za ngozi, maua, matunda, karanga, sukari , kahawa, chai, viungo, kofia, bidhaa za kauri, rangi, kati ya bidhaa nyengine.

Siku ya Alhamisi, katika mkutano uliofanyika Mombasa ulioongozwa na Waziri wa Biashara wa Kenya Betty Maina, ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la EAC, Nchi sita washirika wa EAC zilifikia makubaliano kwamba asilimia 35 ya ushuru huo itatozwa kuanzia Julai 1, 2022.

Hii ina maana kwamba Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania zitapunguza ushuru wa juu kwa waagizaji bidhaa zilizoathirika.

Ushuru utakaotozwa kwa bidhaa zilizokamilishwa kutoka nje kutoka nchi zisizo wanachama unatarajiwa kuchochea uzalishaji wa ndani na ukuzaji wa viwanda.

Chanzo: BBC