Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya viazi mviringo Arusha yang’ang’ania pale pale

Lindege Bei ya chini ni Sh85,000 ambayo nayo haijabadilika.

Thu, 10 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bei ya jumla ya viazi mviringo katika Mkoa wa Arusha imeendelea kung’ang’ania kiwango kilekile cha Sh90,000 kilichorekodiwa Jumatano Machi 2, 2022, jambo linaloashiria hakuna ongezeko la faida kwa wafanyabiashara mkoani humo.

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Machi 9, 2022) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha kuwa gunia la kilo 100 la viazi mviringo linauzwa Sh90,000 katika mkoa huo, bei ambayo inafanana na ile iliyotumika Jumatano ya wiki iliyopita.

Bei hiyo ndiyo bei ya juu kabisa huku bei ya chini ya zao hilo inayotumika leo mkoani humo ikiwa ni Sh85,000 ambapo nayo haijabadilika ukilinganisha na iliyorekodiwa wiki iliyopita.

Hiyo ina maana kuwa wafanyabiashara wa zao hilo hawajaongeza faida ya zao hilo ndani ya wiki moja kwa sababu bei zimebaki zile zile, jambo ambalo pia ni ahueni kwa wanunuzi ambao wakati wote hupendelea bei ishuke.

Viazi mviringo ni miongoni mwa mazao ya chakula yanayotumiwa zaidi na Watanzania hasa kutengeneza chakula cha haraka kama chipsi.

Hata hivyo, bei ya juu ya viazi mviringo inayotumika leo Tanzania Bara imerekodiwa katika mikoa ya Kigoma na Dodoma ambapo gunia la kilo 100 linauzwa kwa Sh110,000 huku bei ya chini ni Sh50,000 ambayo imerekodiwa katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live