Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya sukari yatikisa Bunge, Waziri Mwijage apata kigugumizi

7642 Charles Mwijage Bungeni TZW

Tue, 8 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameshindwa kutoa majibu ya serikali baada ya Mbunge wa Mpendae, Salim Turky (CCM), Kwanini sukari imekuwa ikiuzwa bei ghali upande wa Tanzania Bara tofauti na ilivyo Zanzibar.



Mwijage amesema kuwa sababu ya sukari Tanzania bara kuuzwa ghali sana ni kutokana na gharama za uzalishaji bara kuwa juu sana kuliko Zanzibar, hali ambayo ilipeleka wabunge kutoa sauti za kelele kuashiria kutoridhishwa na jibu hilo.

“Nimejitahidi sana kuelezea suala hili lakini muda hautoshi, Ni kwamba Gharama za uzalishaji sukari bara zipo juu kuliko Zanzibar. Nimepewa muda naomba mniache niwaeleze.Hili suala siyo rahisi kama mnavyofikiria,ndiyo siyo suala rahisi naomba niwaeleze,” alifafanua Waziri Mwijage.

“I am very good in talking, I can talk. Mh. Turky ulipopewa kibali na serikali kuingiza sukari ni kwa nini wewe hukuuza bei rahisi? ameongeza Waziri Mwijage na kurudi kukaa kwenye kiti.

Hata hivyo Turky ametolea mfano soko la dunia amesema kwamba “Sukari kwasasa hivi inauzwa dola 390 ukilipia kodi 25% na VAT 18% sukari hiyo inasimama kwa bei ya sh 65000. Leo Watanzania tunalanguliwa kwa kuuziwa sukari 110000 kwa misingi gani?” alihoji.

Hata hivyo Spika Ndugai aliingilia kati na kusema kuwa “suala hili ni la Msingi sana kwa wananchi wa Tanzania na kwakweli halijapata majibu kwahiyo tutalipanga tena kwenye maswali ya wiki ijayo ili serikali itupe majibu ya kina linapaswa kutolewa majibu ya kina na serikali.”

Loading...
Chanzo: bongo5.com