Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya samaki soko la Feri yazidi kupaa

FERI Bei ya samaki soko la Feri yazidi kupaa

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: mtanzania.co.tz

CHRISTINA GAULUHANGA– DAR ES SALAAM

BEI ya samaki katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri imeendelea kupanda kwa sababu ya hali ya hewa ya upepo ulioanza wiki iliyopita.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa soko hilo, Mubarak Kilima alisema kuwa hali ya hewa imebadili gharama za manunuzi ya samaki na kusababisha baadhi ya wafanyabiashara na hata watumiaji kushindwa kumudu gharama hizo.

Alisema awali ndoo ya samaki kubwa ilikuwa kuanzia Sh15,000 hadi 30,000 lakini kwa sasa imepanda na kufikia Sh 50,000 hadi 90,000.

“Bei ya samaki kwa sasa imepanda kwa sababu ya hali ya hewa iliyochangia uhaba na kusababisha wafanyabiashara wengi kushindwa kumudu gharama ,”alisema Kilima.

Akizungumzia kuhusu ubora wa miundombinu alisema, mazingira kwa sasa yameboreshwa kiasi na upatikanaji wa maji ni wa uhakika.

Alisema hata hivyo Benki ya Dunia imeanza kufanya utafiti katika soko hilo kwa lengo la ukarabati utakaoanza siku za hivi karibuni.

“Benki ya dunia mara baada ya kumaliza utafiti wao kutaanza ukarabati na ujenzi wa kisasa wa soko hilo na ni imani yetu litakuwa linavutia zaidi kulingana na hadhi yake,”alisema Kilima.

Chanzo: mtanzania.co.tz