Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya pamba yatangazwa kupanda maradufu

769b042287a72392a2e0715007921bfb.jpeg Bei ya pamba yatangazwa kupanda maradufu

Mon, 11 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro wameshauriwa kulima pamba kwa kuwa bei elekezi ya serikali imezidi kuongezeka kutoka shilingi 1,050 msimu uliopia hadi Sh 1,560 kwa kilo moja msimu huu.

Katika Wilaya ya Mvomero zao hilo linalimwa katika kata za Doma, Makuyu, Mziha, Kibiti na kata ya Kanga Akitoa mada katika kikao cha wadau wa maendeleo ya kilimo na mifugo cha kujadili mikakati ya kuendeleza kilimo na mifugo kilichofanyika jana wilayani humo Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Mvomero, Alphonce Ngawagala alisema kuna fursa ya kulima zaidi ya kulima pamba mkoani humo.

Ngwawagala alisema bodi ya pamba, Halmashauri ya Wilaya na wataalamu wa kilimo wameendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa zao hilo.

Aidha alisema pia ukubwa wa eneo la uzalishaji umeongezeka kutoka ekari 231 hadi kufikia ekari 850 ambapo alisema kwa upande wa mavuno ya zao hilo kwa Wilaya ya Mvomero katika msimu uliopita yalikuwa kilo 27,500 na katika msimu huu wanatarajia mavuno yataongezeka hadi kufikia kilo 187500.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live