Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya pamba yapanda, wakulima wabaki njia panda

Pamba Cotton.jpeg Bei ya pamba yapanda, wakulima wabaki njia panda

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetangaza rasmi bei elekezi ya ununuzi wa zao la pamba katika msimu wa mwaka 2024/2025 kuwa ni Sh 1,150 kwa kilo moja ya pamba daraja la kwanza na daraja la pili ikiwa ni Sh 575 kwa kilo moja. - Bei hiyo imeongezeka kwa Sh 90 kutoka bei iliyotangazwa msimu wa mwaka jana 2023, ambapo kilo moja ilitangazwa kununuliwa kwa Sh 1,060. - Bei hiyo imetangazwa jana katika kijiji cha Ndoleleji wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga, ambao mbali na kutangazwa kwa bei ulizinduliwa rasmi msimu wa ununuzi wa zao hilo. - Akitangaza bei hiyo, Kaimu Katibu tawala mkoa huo Dafroza Ndalichako amesema kuwa wanunuzi wote wa pamba watatakiwa kununua kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali katika msimu huu. - Ndalichako amesema katika msimu huu wa ununuzi wa pamba, mfumo ambao utatumika kununulia zao hilo kwa wanunuzi wote ni mfumo wa ushirika, ambapo wakulima wote watatakiwa kuuzia pamba yao kwenye vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS). - Hata hivyo wakulima walionekana kutokukubaliana kwa bei iliyotangazwa, wakieleza kuwa bei hiyo ni ndogo na haiwezi kukidhi mahitaji yao kwani wametumia gharama kubwa katika kilimo.

Serikali imetangaza rasmi bei elekezi ya ununuzi wa zao la pamba katika msimu wa mwaka 2024/2025 kuwa ni Sh 1,150 kwa kilo moja ya pamba daraja la kwanza na daraja la pili ikiwa ni Sh 575 kwa kilo moja. - Bei hiyo imeongezeka kwa Sh 90 kutoka bei iliyotangazwa msimu wa mwaka jana 2023, ambapo kilo moja ilitangazwa kununuliwa kwa Sh 1,060. - Bei hiyo imetangazwa jana katika kijiji cha Ndoleleji wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga, ambao mbali na kutangazwa kwa bei ulizinduliwa rasmi msimu wa ununuzi wa zao hilo. - Akitangaza bei hiyo, Kaimu Katibu tawala mkoa huo Dafroza Ndalichako amesema kuwa wanunuzi wote wa pamba watatakiwa kununua kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali katika msimu huu. - Ndalichako amesema katika msimu huu wa ununuzi wa pamba, mfumo ambao utatumika kununulia zao hilo kwa wanunuzi wote ni mfumo wa ushirika, ambapo wakulima wote watatakiwa kuuzia pamba yao kwenye vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS). - Hata hivyo wakulima walionekana kutokukubaliana kwa bei iliyotangazwa, wakieleza kuwa bei hiyo ni ndogo na haiwezi kukidhi mahitaji yao kwani wametumia gharama kubwa katika kilimo. “Kwa hii bei ambayo imetangazwa na Serikali sisi wakulima hatukubaliani nayo, bei ni ndogo sana, hatukutarajia kabisa kutangaziwa bei hii, maana tumefanya kazi kwa kipindi kirefu sana lakini haiwezi kukidhi mahitaji yetu, tunamuomba Rais Samia atuongezee bei kidogo,” amesema mmoja wa wakulima Eliasi Sibani. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live