Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya maziwa kupanda

20396 Maziwa+pic TanzaniaWeb

Wed, 3 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kuanzia sasa, wateja wa maziwa ya kopo watalazimika kuumia zaidi baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitisha kanuni zilizopaisha tozo ya kuingiza maziwa nchini kwa zaidi ya asilimia 1,200.

Agosti 18,  2018 Waziri wa wizara hiyo, Luhaga Mpina amesaini kanuni mpya za huduma za mifugo na bidhaa zake ambazo pamoja na mambo mengine, zimeongeza tozo ya maziwa yanayoingizwa nchini kutoka Sh150 kwa kilo moja mpaka Sh2,000 sawa na ongezeko la asilimia 1,233.

Kutokana na mabadiliko hayo, wateja waliokuwa wananunua kopo la lita moja kwa Sh3,200 sasa hivi watatakiwa kulipa takriban Sh6,000 kwa kiasi hicho.

Viwanda vya kusindika maziwa nchini, takwimu zinaonyesha vinahitaji lita 700,000 lakini uzalishaji uliopo ni asilimia 40 hivyo kulazimu kuagiza kiasi kikubwa kwa ajili ya uzalishaji.

Katika uagizaji huo, Tanzania hutumia zaidi ya Sh165 bilioni kuagiza maziwa kutoka sehemu tofauti duniani. Kabla ya mabadiliko ya kanuni za wizara, ilikuwa rahisi kufanya hivyo lakini mambo yamebadilika hivi sasa.

Mmoja wa wadau wa sekta ya maziwa nchini, Samuel Makubo  anasema hili ni pigo si kwa waagizaji tu bali sekta nzima ya maziwa.

“Uzalishaji nchini haukidhi mahitaji. Viwanda vya maziwa vitashindwa kuagiza malighafi na vikilazimisha basi bidhaa zao zitauzwa kwa bei kubwa. Wananchi tutalazimika kunyang’anyana kiasi kidogo kinachozalishwa nchini,” amesema.

 

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz