Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya mahindi yatikisa Bunge

Maguni Ya Mahindi Bei ya mahindi yatikisa Bunge

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sakata la kuporomoka kwa bei ya mahindi nchini limetinga kwa mara nyingine bungeni baada ya Mbunge wa Mbozi (CCM), George Mwanisongole kutaka Bunge liahirishe shughuli zake ili lijadili suala hilo.

Hoja hiyo imekuwa ikichangiwa na wabunge tangu mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2023/24 uanze Juni 19, 2023 huku Serikali ikitoa ufafanuzi mara kwa mara kuwa haijazuia wafanyabiashara kusafirisha mazao nje ya nje.

Mwanisongole ameomba mwongozo huo leo Juni 22, 2023 baada ya maswali na majibu bungeni.

Amesema Serikali iliweka zuio la kuuza mahindi ambalo limesababisha kuporomoka kwa bei ya mahindi.

Amesema bei ya mahindi katika Mkoa wa Mbeya na jimboni kwake bei imefika ya mahindi imefikia Sh8,000 hadi Sh7,000 kwa debe na inazidi kuporomoka.

“Inavunja moyo wakulima waliojitolea kulima kwa kiwango kikubwa na matokeo yake tunakwenda ambapo gunia la mahindi litauzwa Sh15,000 naomba shughuli za Bunge ziahirishwe tuone ni jinsi gani ya kuishauri Serikali,” amesema.

Hatua ambayo ilimfanya Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kumpatia Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kujibu kuwa hawajazuia mfanyabiashara yoyote wa mazao aliyefuata utaratibu uliowekwa.

Amesema jana wametoa vibali vya kusafirisha mazao nje ya nchi ya tani 20,000 za mahindi na tani 15,000 za unga wa mahindi.

“Bei elekezi ya mahindi kwa Serikali ni Sh800 kwa Sumbawanga Mjini, Mbeya Mjini, Njombe Mjini na Sh600 kwa wilaya zilizoko pembezoni na kwamba Serikali imeipatia NFRA (Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula) Sh320 bilioni na wamefungua vituo vya ununuzi nchini ,”amesema.

Amesema kama mtu wa nje ya nchi anataka kununua mazao nchini aje kufungua kampuni kwa mujibu wa sheria ama anunue kwa kampuni za Watanzania nchini.

Amesema hawawezi kusafirisha mahindi hadi tani 500,000 hadi 700,000 kwa sababu fedha hizo hazionekani katika mfumo wa uchumi wa nchi.

Aidha, amewataka madereva wa mazao ya mizigo kuhakikisha kuwa wanapewa nyaraka zote zinazohusiana na biashara hiyo ikiwemo leseni za biashara na cheti cha kodi ili waweze kuonyesha katika mageti.

Amesema kama mkulima anataka kuuza kwa bei hiyo elekezi, Serikali haizuii kuyauza kwa bei wanayotaka.

Akitoa mwongozo wake Dk Tulia amewataka wabunge kuwaambia wakulima wapeleke mahindi wakauze NFRA kwa sababu bei ni kubwa na fedha zipo.

“Wakienda kule wakakuta fedha hazipo ndio mrudi tena hapa. Mimi nitawapa nafasi kwa sababu bado ipo hapa bungeni. Kawaambieni kukiwa na changamoto basi muilete hoja hiyo hapa,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live