Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya kuku yapanda hadi Sh299,000/-

Kuku Mchungaji Vipande.png Bei ya kuku yapanda hadi Sh299,000/-

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukistaajabu ya Musa, Utayaona ya Firauni. huko mtandaoni kuna mjadala umeibuka sio Bongo bali Toronto, Canada baada ya mdau kuchapisha picha ya bei ya kuku mzima aliyepikwa ‘precooked turkey’ kuonesha anauzwa kwa zaidi ya Sh 299,000 ($120) ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya siku ya Shukrani - Thanksgiving Day.

Tofauti na sehemu zingine zinazoadhimisha siku hii ya Shukrani, ambapo huwa ni Alhamisi ya nne ya Novemba bila kujali tarehe, kwa Canada maadhimisho hayo hufanyika Jumatatu ya pili ya Oktoba-ambayo ni Oktoba 9 mwaka huu.

Ingawa gharama za bidhaa na huduma zimapenda maradufu, wengi hawakutarajia, bei ya kitoweo hicho muhimu kisingeuzwa kwa bei hiyo. Hawakutegemea watapaswa kulipa zaidi ili kushiriki mlo mkuu wa famialia ambapo kuku ni kitoweo muhimu.

Nyama ya bata mzinga ni ghali zaidi ambapo kipande kimoja (robo) ni zaidi ya $60. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live