Geita. Kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia kumepokelewa kwa furaha na wachimbaji wadogo nchini Tanzania walioonekana wakiingia na kutoka kwenye soko kuu la dhahabu mkoani Geita.
Bei ya dhahabu kwenye soko la dunia imepanda kutoka kati ya Sh70,000 na 90,000 kwa gramu moja hadi Sh113,260.
Akizungumza leo Jumatano Agosti 28, 2019 ofisa madini mkazi wa mkoani Geita, Daniel Mapunda amesema kubadilika kwa soko la dhahabu kunatokana na mahitaji ya soko, na kwamba kuanzia Agosti Mosi, 2019 bei imekua ikipanda.
Musa Maliganya na Charles Kazungu, wachimbaji wadogo waliokuwa wakiuza dhahabu zao leo katika la soko hilo wamesema uwepo wa soko hilo umewasaidia kuuza kulingana na bei ya soko la dunia.
“Zamani tulikua tunauza kutokana na alivyopenda mnunuzi lakini hivi sasa tunaangalia bei ubaoni, tunauza na tunapata faida. Awali hatukujua hata bei ya soko la dunia,” amesema Maliganya.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema uwepo wa masoko sita ya dhahabu mkoani humo umesaidia kuongeza uzalishaji kutoka asilimia mbili za awali kwa wachimbaji wadogo hadi 20.
Pia Soma
- Mamia waandamana Dar kushinikiza ndege ya Tanzania iliyozuiwa Afrika Kusini kuachiwa
- Mtifuano wa Dk Bashiru, wapinzani D’ Salaam
- DC Temeke atoa somo kwa wenye watoto viziwiwasioona