Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya Petroli yapanda, Dizeli yashuka Dar

90520 Ewura+pic Bei ya Petroli yapanda, Dizeli yashuka Dar

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (Ewura) nchini Tanzania imetangaza kupanda bei ya kikomo ya mafuta ya petroli jijini Dar es Salaam itakayoanza kutumika leo Jumatano Januari 1, 2020.

Bei hiyo imepanda kutoka Sh2,161 Desemba 2019 hadi Sh2,206 huku bei za dizeli imepungua hadi Sh2,121 kutoka Sh2,125.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany imeeleza kupanda kwa bei hiyo inatoka na kubadilika kwa bei za mafuta katika soko la dunia na ongezeko la gharama za usafirishaji.

“Kwa Januari 2020, bei za rejareja za petroli zimeongezeka kwa Sh45 kwa lita wakati dizeli zimepungua kwa Sh5. Bei za jumla za petroli zimeongezeka kwa Sh44.53” amesema Mchany

Taarifa hiyo imeeleza kutokana na kutopokelewa kwa shehena ya mafuta katika bandari za Mtwara na Tanga bei za mafuta kwa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara hazitakuwa na mabadiliko.

Pa katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma hakutakuwa na mabadiliko ya bei lakini imeshauriwa kununuliwa kwa mafuta ya taa kutoka Dar es Salaam kwa sababu hakuna mafuta ya taa yaliyopokelewa.

“Wamiliki wa vituo vya mafuta katika mikoa ya kusini wanashauriwa kununua mafuta ya taa kutoka Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa zinatokana na gharama za mafuta hayo kutokea jijini Dar na kusafirishwa hadi mkoa husika” amesema Mchany

Ewura imesisitiza kuwa bei za kikomo cha mafuta katika maeneo husika zinapatikana kupitia simu ya mkononi kwa kupiga namba *152*00# kisha kufuata maelezo.

Chanzo: mwananchi.co.tz