Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ndogo yakwamisha mnada wa korosho Mtwara

Korosho.png Bei ndogo yakwamisha mnada wa korosho Mtwara

Sat, 22 Oct 2022 Chanzo: Mwananchi

Wakulima mkoani Mtwara wamekataa kuuza zaidi ya tani 8,000 za wakidai bei ni ndogo. Mnada mmoja ulifanyika wilayani Tandahimba na mwingine wilayani Masasi lakini kote wakulima wameikataa iliyotolewa na wanunuzi.

Katika mnada wa Chama Kikuu cha Ushirika Mtwara, Masasi na Nanyumbu (Mamcu) ulioendeshwa katika Kijiji cha Chingulungu wilayani Masasi, wakulima hao wamekataa kuuza tani 6,513 kwa kati ya Sh1, 800 na Sh2,000 iliyotolewa na wanunuzi.

Akizungumza baada ya kufungua bahasha za wanunuzi 20 waliojitokeza, Meneja wa Mamcu, Bihadia Matipa aliwauliza wakulima iwapo wapo tayari kuuza korosho zao kwa bei hizo na wote kwa pamoja walikataa.

Katika mnada wa Chama Kikuu cha Ushirika Tandahimba na Newala (Tanecu), wakulima pia wamekataa kuuza korosho zao kwa kati ya Sh1,630 na Sh2,011.

Kutofanyika kwa mnada huo katika Kijiji cha Mitondi B wilayani Tandahimba kunamaanisha korosho hizo zitapelekwa katika mnada ujao utakaofanyikia Kijiji cha Nanguruwe wilayani Newala.

Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa mnada huo, Meneja Mkuu wa Tanecu, Mohamed Mwinguku amesema zaidi ya tani 1,610 zitaingizwa sokoni msimu huu.

Amesema katika mnada huo kulikuwa na zaidi ya maombi 16 lakini wakulima wamekataa kuuza korosho hizo kwa bei kati ya Sh1,630 na Sh2,011.

“Kuuza korosho ni makubaliano, mkulima akikubali sisi chama cha ushirika tunauza. Dhamana ya kuuza korosho ni ya mkulima mwenyewe. Nafikiri tuvute subira tuone mnada ujao hali itakuwaje tutazirudisha hizi korosho mnadani wakilidhika na bei,” amesema Mwinguku.

Hii samara ya kwanza kwa wkaulima kukataa kuuza korosho kutokana nakutoridhika na bei.Katika mnada wa kwanza wa msimu wa mwaka 2018/19 uliofanyika Oktoba 23 mwaka 2018 katika Kijiji cha Makukwe wilayani Newala.

Wakulima hao walikataa kuuza korosho zaolicha ya kampuni 15 kujitokeza kununua kwa bei ya juu Sh2,717 huku ya chini ikiwa ni Sh1,711 kwa kilo hivyo mnada kuvunjika.

Chanzo: Mwananchi