Leo ni January 3, 2017 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei mpya elekezi za Mafuta ya Petrol, Diesel pamoja na mafuta ya Taa kwa Mwaka. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia January 3.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godwin Samwel, bei zitakazoanza kutumika leo Petroli imezidi kupanda bei kwa shilingi 8/lita, kupanda huku kumetokana na mabadiliko ya bei katika soko la Dunia.
Pamoja na kutaja bei kikomo za bidhaa mbalimbali za mafuta nchi nzima, EWURA wametaja mambo muhimu ya kuzingatia nakusogezea kama walivyotoa katika taarifa yao ya leo kama ifuatavyo.
Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, yaani Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Disemba 2017. Kwa mwezi Januari 2018, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 8/lita (sawa na asilimia 0.35), Shilingi 34/lita (sawa na asilimia 1.71) na Shilingi 89/lita (sawa na asilimia 4.57) sawia. Vilevile, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 7.56/lita (sawa na asilimia 0.37), Shilingi 33.97/lita (sawa na asilimia 1.81) na Shilingi 88.73/lita (sawa na asilimia 4.85) sawia. Ongezeko la bei za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa limetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na ongezeko la gharama za usafirishaji (BPS Premiums). Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Disemba 2017. Bei za Mafuta ya Taa hazijabadilika kwa sababu hakuna Mafuta ya Taa yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga katika mwezi wa Disemba 2017. Katika toleo hili, bei za rejareja za Petroli na Dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini zimeongezeka kwa Shilingi 60/lita (sawa na asilimia 2.78) na Shilingi 69/lita (sawa na asilimia 3.47), sawia. Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa Shilingi 59.68/lita (sawa na asilimia 2.93) na Shilingi 69.02/lita (sawa na asilimia 3.67). Ongezeko la bei za mafuta ya Petroli na Dizeli katika mkoa wa Tanga linatokana na kuongezeka kwa bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji (BPS premiums). Ifahamike kwamba, sehemu kubwa ya shehena za mafuta yaliyopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam ni zile zenye bei za soko la dunia za mwezi Oktoba 2017 wakati shehena iliyopokelewa katika bandari ya Tanga ni ya bei za soko la dunia za mwezi Novemba 2017. Bei za mafuta katika soko la dunia kwa mwezi Novemba 2017 ziko juu kwa zaidi ya asilimia 6 ikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2017. Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo husika, zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini. Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na kanuni (formula) iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 216/2017 la mwezi Mei 2017. Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika. Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahishisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mafuta ya petroli.
Nimekuwekea hapa chini bei za mafuta kwa nchi nzima kuanzia kesho Jumamosi July 1, 2017.
A: BEI ZA REJAREJA
Mji Bei Kikomo Petroli (Shs/Lita) Dizeli (Shs/Lita) Mafuta Ya Taa (Shs/Lita) Dar es Salaam 2,167 2,018 2,031 Arusha 2,263 2,115 1,995 Arumeru (Usa West) 2,263 2,115 1,995 Karatu 2,281 2,134 2,013 Monduli 2,268 2,121 2,000 Monduli-Makuyuni 2,273 2,125 2,005 Ngorongoro (Loliondo) 2,347 2,200 2,079 Kibaha 2,172 2,023 2,036 Bagamoyo 2,178 2,029 2,042 Kisarawe 2,175 2,025 2,038 Mkuranga 2,177 2,028 2,041 Rufiji 2,195 2,046 2,059 Dodoma 2,226 2,077 2,090 Bahi 2,233 2,084 2,097 Chemba 2,252 2,103 2,116 Kondoa 2,259 2,109 2,122 Kongwa 2,223 2,074 2,087 Mpwapwa 2,227 2,078 2,091 Iringa 2,231 2,082 2,095 Kilolo 2,236 2,087 2,099 Mufindi (Mafinga) 2,241 2,092 2,105 Njombe 2,259 2,110 2,123 Njombe (Kidegembye) 2,280 2,131 2,144
Ludewa 2,297 2,148 2,161 Makete 2,290 2,141 2,154 Wanging’ombe (Igwachanya) 2,257 2,108 2,121 Bukoba 2,382 2,233 2,246 Biharamulo 2,357 2,207 2,220 Karagwe (Kayanga) 2,399 2,249 2,262 Kyerwa (Ruberwa) 2,404 2,255 2,268 Muleba 2,382 2,233 2,246 Ngara 2,348 2,199 2,211 Misenyi 2,391 2,241 2,254 Geita 2,332 2,183 2,196 Bukombe 2,321 2,172 2,185 Chato 2,353 2,204 2,217 Mbogwe 2,370 2,221 2,234 Nyang’hwale 2,347 2,198 2,211 Kigoma 2,398 2,249 2,262 Uvinza (Lugufu) 2,410 2,261 2,274 Buhigwe 2,387 2,238 2,251 Kakonko 2,355 2,206 2,219 Kasulu 2,384 2,235 2,248 Kibondo 2,363 2,213 2,226 Moshi 2,253 2,105 1,984 Hai (Bomang’ombe) 2,256 2,108 1,988 Mwanga 2,246 2,098 1,977 Rombo (Mkuu) 2,269 2,122 2,001 Same 2,239 2,091 1,971 Siha (Sanya Juu) 2,259 2,112 1,991 Lindi 2,226 2,077 2,090 Lindi-Mtama 2,244 2,095 2,108 Kilwa Masoko 2,201 2,052 2,065 Liwale 2,247 2,098 2,111 Nachingwea 2,255 2,106 2,119 Ruangwa 2,257 2,108 2,121 Babati 2,297 2,149 2,029 Hanang (Katesh) 2,307 2,160 2,039 Kiteto (Kibaya) 2,312 2,165 2,044 Mbulu 2,310 2,162 2,041 Simanjiro (Orkasumet) 2,329 2,181 2,061 Musoma 2,346 2,196 2,209 Musoma Vijijini (Busekela) 2,386 2,237 2,250 Rorya (Ingirijuu) 2,354 2,205 2,218 Rorya (Shirati) 2,389 2,240 2,253 Bunda 2,337 2,187 2,200 Butiama 2,342 2,193 2,206 Serengeti (Mugumu) 2,391 2,242 2,255 Tarime 2,357 2,207 2,220 Tarime (Kewanja/Nyamongo) 2,361 2,212 2,225 Mbeya 2,274 2,125 2,138
Chunya 2,284 2,134 2,147 Chunya (Makongolosi) 2,298 2,149 2,162 Ileje 2,287 2,138 2,151 Kyela 2,290 2,141 2,154 Mbarali (Rujewa) 2,258 2,109 2,122 Mbozi (Vwawa) 2,284 2,134 2,147 Momba (Chitete) 2,292 2,143 2,156 Rungwe (Tukuyu) 2,283 2,134 2,147 Morogoro 2,192 2,043 2,056 Mikumi 2,208 2,059 2,072 Kilombero (Ifakara) 2,230 2,081 2,094 Kilombero (Mlimba) 2,252 2,103 2,116 Kilombero (Mngeta) 2,242 2,092 2,105 Ulanga (Mahenge) 2,241 2,091 2,104 Malinyi 2,251 2,102 2,115 Kilosa 2,211 2,061 2,074 Gairo 2,211 2,061 2,074 Mvomero (Wami Sokoine) 2,203 2,054 2,066 Turiani 2,217 2,068 2,081 Mtwara 2,240 2,090 2,103 Nanyumbu (Mangaka) 2,288 2,139 2,152 Masasi 2,265 2,116 2,129 Newala 2,272 2,122 2,135 Tandahimba 2,265 2,115 2,128 Mwanza 2,317 2,168 2,181 Kwimba 2,353 2,204 2,217 Magu 2,325 2,176 2,189 Misungwi 2,323 2,173 2,186 Sengerema 2,350 2,200 2,213 Ukerewe 2,377 2,227 2,240 Sumbawanga 2,340 2,191 2,203 Kalambo (Matai) 2,347 2,198 2,211 Nkasi (Namanyele) 2,353 2,204 2,217 Katavi (Mpanda) 2,375 2,226 2,238 Mlele (Inyonga) 2,353 2,204 2,217 Songea 2,291 2,141 2,154 Mbinga 2,324 2,175 2,188 Namtumbo 2,320 2,171 2,183 Nyasa (Mbamba Bay) 2,326 2,177 2,190 Tunduru 2,349 2,200 2,213 Shinyanga 2,296 2,147 2,160 Kahama 2,310 2,160 2,173 Kishapu 2,324 2,175 2,188 Simiyu (Bariadi) 2,337 2,188 2,201 Busega (Nyashimo) 2,330 2,181 2,194 Itilima (Lagangabilili) 2,340 2,191 2,204 Maswa 2,329 2,180 2,192 Meatu (Mwanhuzi) 2,336 2,187 2,199 Singida 2,258 2,109 2,121 Iramba 2,270 2,121 2,134 Manyoni 2,242 2,093 2,106 Ikungi 2,253 2,104 2,117 Mkalama (Nduguti) 2,282 2,133 2,146 Tabora 2,321 2,172 2,185 Igunga 2,275 2,126 2,139 Kaliua 2,339 2,190 2,203 Ulyankulu 2,333 2,184 2,197 Nzega 2,286 2,137 2,149 Sikonge 2,333 2,184 2,197 Urambo 2,334 2,185 2,198 Tanga 2,206 2,059 1,938 Handeni 2,227 2,079 1,959 Kilindi 2,242 2,094 1,974 Korogwe 2,219 2,071 1,950 Lushoto 2,228 2,080 1,960 Mkinga (Maramba) 2,213 2,066 1,945 Muheza 2,211 2,064 1,943 Pangani 2,213 2,066 1,945
B: BEI ZA JUMLA
Bei za Jumla – DSM Petroli (Shs/Lita) Dizeli (Shs/Lita) Mafuta ya Taa (Shs/Lita) Bei Kikomo 2,056.41 1,907.12 1,920.00
Bei za Jumla –
TANGA Petroli (Shs/Lita) Dizeli (Shs/Lita) Mafuta ya Taa (Shs/Lita) Bei Kikomo 2,095.46 1,947.93 1,827.17 Mhandisi Godwin Samwel
KAIMU MKURUGENZI MKUU
EWURA
VIDEO: ALICHOONGEA RAIS MAGUFULI KWA BABU SEYA NA WATOTO WAKE IKULU LEO