Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei mpya za Mafuta Balaa

Ewura Pic Kupanda kwa Bei ya Mafuta

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waendesha magari sasa, watalazimika kukamua zaidi mifuko yao baada yaMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kutangaza bei mpya ya mafuta ya petroli ambayo imekuwa ikipanda katika kipindi cha mwezi mmoja.

Marekebisho ya hivi karibuni yalitekelezwa Julai 1, 2021 huku serikali ikiwa inataka kukusanya Shilingi 100 kutoka katika kila lita ya mafuta ambayo inaenda sambamba na bajeti ya Sh36.68 trilioni kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Petrol itauzwa kwa sh 2,427 kwa lita huku ya dizeli ikiuzwa shiling 2,251 kwa lita na mafuta ya taa shilingi 2,176 katika mkoa wa Dar es Salam.

Kwa Mujibu wa Ewura mabadiliko ya bei yanatokana na mabadiliko ya soko la mafuta la dunia na Mfumo wa Ununuzi (BPS).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live