Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei elekezi za vifurushi kuanza kutumika leo

Kilaba 3 Ed Bei elekezi za vifurushi kuanza kutumika leo

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kanuni hizo ziliandaliwa kufuatia maoni 3,278 yaliyotolewa na wananchi kuhusu vifurushi hivyo.

Baadhi ya mitandao ya simu jana iliwataarifu watumiaji wake juu ya hayo mabadiliko yanayoanza leo.

Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji TCRA, Dk. Philip Filikunjombe, alisema baadhi ya changamoto walizokuwa wakikutana nazo watumiaji wa huduma za simu ni pamoja na gharama za vifurushi kuwa juu na vifurushi vya data kubadilika mara kwa mara.

Dk Filikunjombe alisema vilevile watumiaji walilalamikia kutumiwa ujumbe mfupi wa simu bila ridhaa yao, watumiaji kupoteza GB katika bando pale muda wa bando unapokwisha ilhali bado GB hazijaisha, utitiri wa bando zinazotolewa na watoa huduma pamoja na kwisha haraka.

Chanzo: ippmedia.com