Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei elekezi ya sukari ni Tsh 2700/= hadi Tsh 3200/=

Sukari2 Bei ya sukari

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema inaendelea kuchukua hatua ili kudhibiti tatizo la bei ya sukari nchini, ambapo imeruhusu uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi na kwamba shehena ya kwanza ya sukari itaanza kuingia nchini mnamo Februari 15, 2024.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe, wakati akizungumza na wananchi mkoani Arusha kupitia simu ya mkononi ya Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, ambapo amebainisha kuwa wametoa vibali vinavyoruhusu zaidi ya tani laki 1, kuagizwa kutoka nje.

Bashe amesema sio kwamba ndani ya nchi hakuna sukari bali kuna wafanyabiashara ambao wanatengeneza upungufu wa bidhaa hiyo na kwamba Serikali kupitia Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa kushirikiana na Bodi ya Sukari nchini wanaendelea na oparesheni ya kuwakamata wafanyabiashara wenye tabia hizo.

Aidha, Bashe ametaja bei elekezi ya sukari nchini ni kati ya Tsh. 2700/= hadi 3200/= kulingana na eneo husika, ambapo ameeleza kuwa, licha ya kutoa vibali vya kuingiza sukari nchini, lakini wataendelea kulinda viwanda vya ndani na endapo viwanda hivyo vitatumia nafasi hiyo kuwaumiza wananchi, Serikali haitosita kuondoa sera hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live