Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei elekezi ngano ya wakulima yatajwa

B9ff833cb95d21f923a1993e01665a9d Bei elekezi ngano ya wakulima yatajwa

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

S ERIKALI imekubaliana na sekta binafsi kuboresha uzalishaji wa ngano nchini huku ikitoa bei elekezi ya Sh 800 kwa kilo ya ngano.

Aidha, aimeamuru wanaomiliki mashamba ya serikali ya ngano ambayo hayalimwi wayarudishe. Waziri wa Kilimo Profesa, Adolf Mkenda alisema hayo kwenye mkutano wa wadau wa tasnia ya ngano.

Alisema Tanzania imekuwa ikitumia Sh trilioni 1.03 kuagiza ngano kutoka nje ya nchi. Alisema serikali imeweka mikakati ya kuamsha tena ngano na shayiri kupunguza kuagiza mazao hayo kutoka nje ya nchi.

Alisema miaka mitano iliyopita, zaidi ya tani 1,800 za ngano ziliagizwa kutoka nje ya nchi huku uzalishaji wa ndani ukiwa ni tani 60,000 hadi 70,000 licha ya wataalamu kusema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha ngano katika nchi za Afrika Mashariki.

Profesa Mkenda alisema wakulima wamekuwa wakiacha kulima ngano kutokana na kutumia gharama kubwa huku bei ikiwa chini.

Alisema kwa Tanzania kwa hekta moja wanapata tani 1.5 hadi 0.7 lakini wa wazalishai wa nje wanapata tani hata tano kwa hekta, na bei ya soko la Tanzania ni Sh 600 kwa kilo.

“Bei iko chini wakulima hawana hamasa na kiwango cha ubora kiko chini, tusipoyamaliza haya kilimo hakitakuwa endelevu, leo tunaanza safari ya kunyanyua tena zao la ngano na shayiri,” alisema

Alisema, “Tumekubaliana na wanunuzi wenye viwanda vya kusindika ngano kuwa, bei ya chini kabisa iwe Sh 800, hapa ndipo sekta binafsi wakubali maumivu kidogo, wakulima wanaotaka kulima ngano kwa bei hii watalima ngano.”

Aidha aliwataka sekta binafsi kuangalia namna ya kuwaunganisha wakulima wenye mashamba madogo madogo kujiunga kwenye mfumo wa ushirika ili waweze kuzalisha ngano nyingi.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya alisema Tanzania imekuwa ikitumia trilioni 1.03 kwa ajili ya kuagiza ngano kutoka nje ya nchi.

“Tanzania ina hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo lakini ni hekta milioni 10.8 ndio zinatumika inafika sehemu tunaagiza ngano hii ni aibu haifai kuifumbia macho.

Tunatakiwa na sisi tuwe mabingwa wanaozalisha ngano kwa wingi sana,” alisema.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda alisema sasa mkoa wa Dodoma umeingia miongoni mwa mikoa inayokwenda kuzalisha ngano.

“Utafiti ulifanyika na matokeo yamekuwa mazuri na Dodoma inaingia kwenye uzalishaji wa ngano,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz