Waziri wa Ujenzi,.Innocent Bashungwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Mohammed Besta kukamilisha usanifu wa kina wa Barabara ya Mkata- Kwamsisi Km 36, ifikapo desemba 31 mwaka huu.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua athari za mvua za vuli mkoani Tanga Novemba 22 , 2023 Bashungwa amesema fedha za mradi huo zipo tayari hivyo kinachotakiwa kazi ya usanifu ifanyike haraka ili ujenzi uanze maramoja.
" Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameashatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara hii hivyo kazi ya usanifu ikikamilika ujenzi uaanze haraka," amesisitiza Bashungwa.
Amezungumzia umuhimu wa watendaji wa TANROADS wa ngazi zote kushirikiana na Mamlaka za Serikali ya mitaa ili kurahisisha ufuatiliaji wa kazi za wakandarasi na kuwezesha kufutilia haki za watumishi katika miradi ya ujenzi na hivyo kuleta tija katika utekelezaji wake.
Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohammed Besta amesema wamejipanga kuhakikisha usanifu unakamilika kwa wakati na taratibu za kumpata mkandarasi wa ujenzi huo unakamilika mapema iwezekanavyo. -