Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashungwa aeleza mchango wa sekta za wizara kwa uchumi

7d11c7bd807eec607af600c0bd2ba1c4.png Bashungwa aeleza mchango wa sekta za wizara kwa uchumi

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, amesema, sekta za wizara hiyo zina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

Aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akiwasilisha muundo na majukumu ya wizara hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Alisema, sekta ya sanaa na michezo zilichangia ongezeko la pato la taifa na kwamba, mwaka 2018 shughuli za burudani zilichangia pato hilo kwa asilimia 13.7 na kushika nafasi ya kwanza na mwaka 2019 shughuli hizo zilichangia asilimia 11.2 na kushika nafasi ya tatu.

“Tunashukuru kamati kwa kutupa mawazo chanya ambayo yatasaidia kuboresha na kuendeleza sekta hizi, naahidi mimi pamoja na timu yangu tutayafanyia kazi mawazo mliyotupa na tayari tumeanza kufanya hivyo katika sekta zote” alisema Bashungwa.

Alisema wizara imeanza kutengeneza Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Michezo na ujenzi wa uwanja wa michezo na Sanaa jijini Dodoma. Bashungwa alisema, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameanza kushirikiana namna ya kukusanya mapato ya kazi za sanaa kupitia njia za kidijiti.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stasilaus Nyongo, aliipongeza wizara hiyo kwa mikakati ya kusaidia sekta inazozisimia, na akashauri wizara hiyo iongeze ubunifu katika kukusanya mapato ya serikali kupitia sanaa na michezo.

Chanzo: habarileo.co.tz